Wednesday, 21 February 2018

Katibu Hamasa Uvccm Amtaka Lema,Meya kukabidhi Jimbo

Katibu Hamasa wa Umoja wa Vijana Uvccm Mkoa wa Arusha Ndg.Omary Lumato Amewapongeza madiwani hao  wawili wa Chadema waliojivua nyadhifa zao na  kujiunga na Ccm.

Akizungumza na mwandishi wetu Ndg.Lumato Alisema

"Namtumia tu salamu Mbunge wa Arusha mjini Mh: Lema  kuwa kwa sasa siasa zake za maandamano  zimepitwa na wakati na wananchi wa Arusha wanahitaji maendeleo na wala sio maandamano hivyo ajiandae tu kukabidhi Jimbo hili kwa Ccm pia tunamkaribisha  kujiunga na Chama cha Mapinduzi kabla ya Uchaguzi mkuu 2020."

Ndg.Lumato alisisitiza kuwa 

 "Hawa madiwani waliojiuzulu waliona hawawezi kutekeleza ahadi walizo ahidi kwa wananchi wao kwani kile chama chao walichokuwepo hakina Ilani  hivyo wakaona wamuunge mkono Rais wetu Mpendwa  Dr John Pombe Joseph Magufuli.

Pia ilani waliyokuwa wanaitekeleza ni ya chama cha mapinduzi hivyo nawasihi madiwani wengine akiwemo rafiki yangu mstahiki Meya Calist Lazaro  na yeye tunamkaribisha kuja kujumuika nasi katika chama cha Mapinduzi.


Sisi kama vijana wa Mkoa wa Arusha sasa tunaingia Kazini tutahakikisha tena tunawapiga Tano bila (5-0) yani ngorongoro 3 bila na Arusha Mjini 2 bila na hii ni salamu tosha kwa chaguzi hizi ndogo zinazo kuja wajiandae kukabidhi hizo kata kwa chama cha mapinduzi. 


#TUKUTANE KAZINI 

No comments:

Post a comment