Saturday, 24 February 2018

Jumuiya ya wazazi Arusha Mjini Wapokea wanachama wapya


 Jumuiya ya Wazazi Wilaya Arusha Mjini wakiishirikiana na Mbunge wa Vitimaalum Mh: Catherine Magige  wamewapokea wanachama wapya kutoka Tawi la Shirikisho la Vyuo la Chuo Kikuu cha Arusha University.

Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama hao Mh: Magige Alisema
" Nimejitolea kuwa mlezi wenu na kuwasaidia baadhi vitendea kama Kompyuta,na Ofisi,
Nitataka kupata orodha yenu ili popote nitakapopata fursa nitakuwa nawasemea vijana wa vyuo maana Rais wetu Mpendwa Dr.John Magufuli anatoa sana fursa kwa vijana wasomi.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Arusha Mjini Ndg.Ally Juma Mwinyimvua amewasisistiza wanachama hao kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi (Ccm) na kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli

Pia Mjumbe wa Baraza kuu la wazazi Taifa  Ndg.Victor Mollel amewataka wanavyuo kutumia Taaluma zao katika kuelimisha mazuri yanayofanywa na Serikali hii hususani ongezeko la vyuo ,Barabara,huduma za Afya maji safi na salama.
Mbunge wa Viti Maalum Mh : Catherine Magige akikabidhi Kadi ya uwanachama kwa mwanachama mpya wa chama hicho.

No comments:

Post a comment