Chadema walalamikia kuchezewa rafu Kinondoni


Chadema wameweka bayana mambo ambayo yanaendelea katika vituo vya kupigia kura hasa linalohusu viapo vya mawakala.

Mkuu wa Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila amesema walianza kupokea viapo hivyo tangu jana majira ya saa kumi jioni.

" Viapo ambavyo tumevipata jana vilikuwa ni kopi, maana inaonekana saini ya Msimamizi Mkuu imesainiwa katika kiapo kimoja kisha vikawekwa katika viapo vingine.

" Baada ya kuapa inatakiwa barua ya mkurugenzi wa uchaguzi kumtambulisha wakala kwa msimamizi wa kituo, na mpaka jana saa tano usiku tulikua hatujapata barua hadi tulipoenda kwa Mkurugenzi usiku huo akasema tayari ameshatoa kwa watendaji wa kata, tumeenda Biafra watendaji wanasema hawajapata," Alisema Kigaila.

Alisema waliendelea kupambana hadi asubuhi hii ambapo mawakala wao walipoenda kwenye vituo vyao wakazuiwa hadi saa mbili ndio wakapewa barua.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: