Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga akizungumza na wananchi na wanakikundi cha Kijiji cha Mahenge Wilayni kilolo mara baada ya kujioena kazi zinazofanywa na mradi wa CoFOREST kwa kushirikaiana na Wananchi.

Mkurugenzi wa Shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania (TFCG) Bwana Emmanuel Lyimo akitoa salamu za shirika lake na kazi wanazofanya katika kuhifadhi misitu nchini.

Meneja mradi wa Mkaa Endelevu bwana Charles Lyimo akifafanua hatua ambazo mradi umepitia na faida zinazoonekana kwenye maeneo yote ya mradi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga akifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa kamati ya maliasili ya Kijiji naman wanavyogawa vitalu vya uchomaji wa mkaa pampja na ukataji wa mbao.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga akiangalia baadhi ya miti iliyohifadhiwa ndani ya m situ wa asili wa Kijiji ambayo wananchi wa Kijiji hicho wanasema kuwa ni dawa za kutibu magonjwa mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga akiwa kwenye picha ya pampoja na kamati ya maliasili ya Kijiji hicho cha Mahenge.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa diwani wa kata hiyo kama sehemu ya shukrani na upendo kwa kuwatembelea.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendigaakipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Mahenge bwana Saidi Muhina kwa niaba ya wanakijiji hicho.
Ukaguzi ukiendelea.

Kazi zikiendelea kwenye msitu huo.
Safari ya ukaguzi wa msitu huo ikiendelea


 

Na Calvin Gwabara, Iringa


MKUU wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga amewataka Wananchi wa Mkoa huo kuzitunza na kuzilinda rasilimali zinazwazunguka kwenye maeneo yao na kwa kufanya hivyo atahakikisha wananufaika nazo kwa kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi na viongozi alioambatana nao kujionea furasa na mbinu zinazotumiwa na Kijiji cha Mahenge Wilayani Kilolo Mkoani humo  kinavyotekeleza Mradi wa kuhifadhi misitu kupitia biashara endelevu ya mazao ya misitu (CoFOREST) unaotekelezwa na Mjumita na TFCG kwa ufadhili wa kwa ufadhili wa Shirika la  Maendeleo la Uswis (SDC).

“Nyinyi hapa mmezungukwa na rasiliamali misitu na wadau wetu TFCG na MJUMITA wamewajengea uwezo mzuri wa kulinda misitu hiyo na kuivuna kwa njia endelevu kwa manufaa ya kizazi hiki na kizazi kijacho hivyo hakikisheni mnasimamia mpango huu ili mnufaike kama ambavyo vijiji vya awali mradi ulipoanzia vunavyonufaika na kupunguza utegemezi kwa halmashauri na serikali ya mkoa itahakikisha inashirikiana na wadau na watafiti ili kuzitumia tafiti hizi nzuri zenye tija kwa Wananchi na Taifa letu” alisitiza Mhe. Sendiga.

Amesema kazi hii kubwa uinayofanywa na wadau hawa inalenga kuunga jitihada kubwa za serikali katika kuhifadhi misitu yetu ya asili nchini kwa kuleta miradi na tafiti zenye tija kwa taifa na kutokana na uhakika huo ndio maana wadau hawa wamepata kibali cha kutekeleza mradi huu mzuri nchini hivyo ni jukumu lenu wote kuwaunga mkono katika uteklezaji wa mradi huu wilayani Kilolo.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Iringa amefafanua kuwa Mkoa wa Iringa kupitia misitu yake na mabonde oevu unachangia katika upatiakaji wa maji kwenye miradi mikubwa ya kimkakati kama vile bwala la kufua umeme la Kidatu, Bwala la kufua umeme la Mwalimu Nyerere ambalo ujenzi wake unaendelea hivyo Wana Iringa wakiharibu misitu na vyanzo vya maji wataharibu mipango mikubwa ya Serikali yenye tija kwa Taifa.

“Niwapongeze sana TFCG na MJUMITA kwa kazi kubwa ya na nzuri ya kwajengea uwezo wananchi kwenye Kijiji hiki cha Mahenge kufanya mpango wa matumizi bora ya ardhi na kuleta mbinu hii bora na endelevu ya kusimamia misitu ya vijiji na uvunaji endelevu wa Mazao ya misitu kama vile Mkaa na Mbao kwa faida ya kizazi hiki na kijacho maana bila kufanya hivi rasilimali hizi sitabakia kuwa historia lakini ni lazima na sisi tuwarithishe vizazi vijavyo kama ambavyo sisi tumerithishwa” alieleza Mkuu huyo wa Mkoa wa Iringa.

Awali akitoa salamu za Shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania (TFCG) Mkurugenzi wa shirika hilo Bwana Emmanuel Lyimo amesema  shirika lao lina mikakati mablimbali ikiwemo kusaidia usimamizi shirikishi wa misitu  kutekeleza sera ya misitu ya mwaka 1998 na sharia ya misitu ya mwaka 2002 namba 14 ambayo imeshusha uhifadhi kwa jamii hivyo kama TFCG wanashiriakiana katika kuhifadhi misitu ya asili ambayo watu wengi wanaona kama haina thamani kwakuwa hawana manufaa nayo.

“Misitu mingi ya asili imebadilshwa na kufanywa misitu ya kupandwa hasa baada ya jamii kuimaliza misitu ya asili kwa kuona hawana faida nayo lakini ukiangalia vizuri utaona misitu ya kupadwa haiwezi kwa na bayoanuai nyingi na uoto kama ilivyo misitu ya asili na ndio maana tukaja na mbinu hii ya jamii kuhifadhi misitu yao ya asili ya vijiji na kunufaika nayo kwa kupata motisha” alieleza Lyimo.

Mkurugenzi huyo wa TFCG amesema mkakati wao mwingine ni katika kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa jamii na mashule,Ushawishi na utetezi katika kuhamasisha serikali kutekelza sera zake,Utafiti na mkakati mwingine ni kuwezesha jamii kupata maendeleo kwa njia mbalimbali kwa kuongeza kipato katika maeneo yao kupitia fursa zinazowazunguka kama kilimo hifadhi, Ufugaji nyuki,Kilimo cha bustani na upandaji wa miti.

Kwa upande wake meneja mradi wa Mkaa Endelevu bwana Charles Lyimo amesema  mradi huo sasa umetimiza Muongo mmoja toka kuanzishwa kwake mwaka 2012 Mkoani Morogoro kwenye vijiji kumi vya Wilaya ya Kilosa awamu ambayo iliisha mwezi wa 11 mwaka  2015.

“Kutokana na mafanikio mazuri ya mradi Serikali na wadau waliomba muda wa utekelezaji uongezwe ndipo ikapatiakana awamu ya pili kuanzia mwezi wa 12 mwaka 2015 hadi mwezi wa 11 mwaka 2019 na wilaya zikaongezake kutoka Wilaya moja ya Kilosa na kwa Wilaya tatu yaani Mvomero,Kilosa na  Morogoro  hivyo mradi kuwa na vijiji 30 katika Mkoa wa Morogoro” alifafanua Bwana Lyimo.

Ameendeea kusema kuwa kutoka na mafanikio pia kwenye vijiji hivyo vya Wilaya za Mvomero na Morogoro wakapata awamu ya tatu ambayo imeongeza Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa,Wilaya ya Ruangwa,Liwale na Nachingwea Mkoani Lindi na hivyo awamu hiyo ya tatu inayoishia mwaka huu 2022 mradi umefikia Wilaya saba na Mikoa mitatu.

“Mradi unalenga kuweka usimamizi shirikishi wa misitu ambao utaleta mabadiliko chanya ya kiuchumi,Kiutawala kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kama vile Mkaa,Mbao,Utalii na mazao mengine mengi ya misitu lakini mabadiliko hayo tunataka  yachochee jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi” alifafanua Meneja Mradi bwana Charles.

Amesema kuwa awamu hii ya tatu ya mradi inalenga kuwajengea uwezo wadau waweze kuchukua mfumo huu wa mradi waweze kuutekeleza usimamizi na uhifadhi shirikishi wa misitu ya asili ambayo itapelekea kuongeza motisha kwa jamii katika kumiliki na kuisimamia misitu hiyo ya asili.

“Mhe. Mkuu wa Mkoa ukitembelea vijiji kwenye wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro vijiji vimepata maendeleo makubwa sana kutokana na usimamizi wa msitu mfano Kijiji kuwa milioni 300 kwenye akaunti yake kwa mwaka sio kitu cha ajabu kabisa maana wengine wajenga madarasa,Barabara,Zahanati na kukatia kila mwanakijiji NHIF iliyoboreshwa kwa kutumia rasilimaliza zao za misitu kwa uendelevu na sasa wanaona faifa ya misitu” alieleza bwana Charles.

Meneja huyo amehimiza kutanua shughuli za mradi kwenye wilaya zingine za Mkoa wa Iringa na mikoa mingine nchi nzima ili faida hizo zienee na kuendelea kote maana tayari mradi unafikia mwisho ufadhili wake lakini wapo wataalamu waliojengewa uwezo kupokea kijiti kwenye wilaya kupitia mapato ya ndani ya halmashauri na mwisho watunze misitu nchini.

Kupitia mradi huo tafiti mbalimbali zimefanyika na nyingine zinaendelea kufanyika kwenye vijiji ambavyo vinatekeleza mradi na miongoni mwa tafiti hizo ni zile zinazofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kuangalia masuala mbalimbali yanayohusu jinsia katika kunufaika na rasilimali za misitu lakini tafiti nyingine ambayo inafanywa na watafiti kutoka SUA ni ile inayoangalia kasi ya uchupuaji na ukuaji wa miti inayoota kwene visiki ambavyo miti ilikatwa ili mwisho kuwepo na Ushahidi wa kisayansi na mapendekezo yenye Ushahidi kuhusu mfumo huo.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: