Na John Walter-Babati

Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amekabidhi zawadi mbalimbali  kwa kituo cha kulelea watoto Yatima na waishio katika mazingira magumu cha Manyara Holistic Center (MAHOCE)kilichopo Kata ya Bagara mjini Babati.

Zawadi zilizokabidhiwa kwa Yatima na waishio katika Mazingira magumu ni pamoja na mchele, mchele, mafuta ya kupikia,mafuta ya kupaka,sukari, sabuni, unga,Miswaki na dawa za meno pamoja  na vitu vingine. 

Akikabidhi msaada huo Mkuu wa wilaya amesema ametoa zawadi hizo ili watoto hao wapate chakula na kufurahia sikukuu ya Idd El Fitri kama watoto wengine kwa kuwa anaguswa na kutambua uwepo wa watoto Yatima na waishio katika Mazingira magumu waliopo wilayani hapo.

Amesema kuwa lengo la Serikali kuweka Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali inayosimamia vituo hivyo,uanzishwaji na uendeshwaji wake ni kuhakikisha kuwa watoto wanaolelewa katika vituo hivyo wanalelewa kwa kuzingatia utaratibu na kwamba ataendelea kuwasaidia katika mambo mbalimbali.


Liberia Vendelunus,Nicodemus Daniel na Niwael Elia  kwa niaba ya watoto wenzao  walimshukuu Mkuu wa wilaya ya Babati, Lazaro Twange kwa msaada huo na wakaomba msaada wa namna hiyo usiwe wa mwisho bali uwe endelevu kwani wanapopata wageni wanao watembelea wanafarijika na kujiona kama watoto wengine waliopo na familia zao.
Share To:

Post A Comment: