Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa  amewanyooshe kidole viongozi wa Halmashauri ya Wilaya na Muheza na Bumbuli kwa kushindwa kukamilisha miradi ya Elimu kwa wakati ilihali fedha za utekelezaji walishapokea muda mrefu.


Akizungumza katika kikao na Viongozi wa Mkoa wa Tanga kilichofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Tarehe 13.05.2022 amesema Halmashauri za Muheza na Bumbuli wahakikishe wanarekebisha mapungufu yaliyopo kabla hajawatembelea kwenye maeneo yao.


Muheza mmepata fedha Takribani shilingi Bil.1 za ujenzi wa shule ya Sekondari lakin mpaka leo hamjakamilisha ujenzi na naskia majengo yaliyopo hayajazingatia ubora na Bumbuli mmepata shilingi Mil.470 mpaka sasa hamjaanza ujenzi wa shule ya Sekondari hizo fedha zikirudi hazina mwishoni wa mwaka sitamuelewa yeyote na ntashughulika naye ipasavyo.


Nendeni mkajipange muone namna gani mnaweza kutekeleza miradi hii kwa haraka na ubora kabla sijatembelea maeneo yenu kwa sababu nikija huko itakua habari nyingine.


Pia Mhe. Bashungwa alisisitiza kuwa  Viongozi waache mivutano na malumbano yasiyo na tija badala yake wajielekeze kwenye majukumu ya msingi yaliyowaweka Madarakani.

Share To:

Post A Comment: