Na Mustafa Leu. 
 TAASISI ya kusanifu mitambo ya kihandisi,kuhamilisha teknolojia na kutoa huduma ya kiufundi kwa viwanda ( TEMDO ) mkombozi wa wakulima wa miwa imejizatiti kumuinua mkulima kiuchumi..


Mkurugenzi mkuu wa (Temdo) Profesa Fredirick Kahindi,amesema taasidi hiyo imebuni na kusanifu mtambo wa kisasa wa kuchakata na kukamuwa miwa kwa ajili ya kuzalisha sukari nchini. Utengenezaji wa mitambo hiyo inatokana na kuwepo mahitaji makubwa kutokana n.a. wakulima wa miwa kukosa sehemu ya kuchakata miwa yao baada ya kuvunwa. 



 

Anasema ukosefu wa mitambo ya kuchakata miwa imekuwa ni changamoto ya muda mrefu na ni kikwazo kikubwa cha kumuinua mkulima wa zao hilo hali hiyo ndiyo iliyoisukuma taasisi hiyo kubuni na kusanifu mitambo hiyo Usanifu na ubunifu wa mitambo hiyo unatokana na Temdo kupata ufadhili kutoka Tume ya yaifa ya Sayansi na teknolojia COSTECH,ili kutatua changamoto za upungufu wa mitambo unaowakabili wakulima wa Miwa na Mazao mengine ya kibiashara nchina. 


 Anasema kwa kipindi kirefu wakulima wa Miwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya miwa yao kushindwa kuchakatwa kwa wakati kutokana na ukosefu wa mitambo kutokana na. kutegemea viwanda vya Sukari ambavyo vina mashamba ya Mila n.a. kipaumbele kinatolewa kwa mid a ya viwanda na wakikamiliza ndipo miwa ya wakulima ichakatwe 


 Profess Kahindi ,anasema katika nchi yetu yapo mabonde mengi ya kulima kilimo cha zao miwa kwa ajili ya kuzalisha sukari nchini na wakulima wanakuwa wakikutana na. changa moto wakati wa mavuno kwa kukosa pa kupeleka miwa yao ili iweze kuchakatwa na kukamuliwa sukari. Wakati wanapokuwa wakisubiri miwa yao kuchakatwa miwa huwa inanyauka na kupungua thamani na hata inapoaanza kuchakatwa haiwezi kutoa sukari nyingi kwa kuwa imesha nyauka  

Anasema ,inabuniwa na kutengenezwa kulingana na. mahitaji na lengo la kutengeneza mitambo hiyo
ni kuongezat tija na hivyo kuinuka kiuchumi. Mbali na kutengeneza mitambo ya kukamua miwa pia Temdo,inasanifu na kubuni mitambo ya mazao mengine ikiwemo Alizeti na mkonge 

 Pia Temdo,inasanifu ,kubuni na kutengeneza vifaa Tiba kwa kwa ajili ya Zahanati,Vituo vya afya na. Hospitali
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: