Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge akielekeza jambo wakati akikagua  ujenzi wa Wodi ya dharura (EMD) katika Hospitali ya Wilaya Kiomboi wilayani Iramba mkoani hapa katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo  ya Sekta ya Elimu, Afya na Maji aliyoifanya leo.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda.

Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge akikagua  ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kisiriri wakati wa ziara hiyo. Kushoto ni Mhandisi wa Wilaya hiyo Profiri Modaha.

Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda wakiongoza ukaguzi wa Kituo cha Afya cha Kisiriri.

Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge akielekeza jambo wakati akikagua  ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Maluga.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda akitoa taarifa ya miradi inayotekelezwa wilayani humo mbele ya mkuu wa mkoa katika kikao kilichofanyika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya wilaya hiyo..

Kikao cha kupokea taarifa kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Katibu Tawala wa wilaya hiyo Pius Sangoma akiwatambulisha watumishi wa wilaya hiyo wakati wa kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii Jane Mkoma akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Charles Gunah akizungumza kwenye kikao hicho.

Kaimu Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Rachel Kanael akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Muonekano wa majengo ya Kituo cha Afya cha Kisiriri kinachoendelea kujengwa.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Hussein Sepoko akitoa taarifa ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kisiriri. Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba, Pius Sangoma.

Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge akielekeza jambo wakati akikagua  ujenzi wa Kituo cha Afya Kisiriri.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Kiomboi, Abel Mafuru akitoa taarifa ya ujenzi wa ujenzi wa Wodi ya dharura (EMD) katika Hospitali ya Wilaya Kiomboi na ujenzi wa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU)

Ukaguzi wa ujenzi wa Wodi ya dharura (EMD) katika Hospitali ya Wilaya Kiomboi na ujenzi wa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) ukifanyika.
Ukaguzi wa mradi wa Maji katika Kijiji cha Maluga ukifanyika.
Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijiji (RUWASA) Wilaya ya Iramba Mhandisi, Ezra Mwacha akitoa taarifa ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Kijiji cha Maluga.

Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijiji (RUWASA) Mkoa wa Singida, Mhandisi Lucas Japhary akichangia jambo wakati wa ukaguzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Maluga.



Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kukamilisha miradi yote ya maendeleo  wilayani humo ambayo Serikali imetoa fedha nyingi kuitekeleza.

Dk. Mahenge ametoamaagizo hayo leo katika ziara yake kikazi ya siku moja ya kukagua baadhi ya miradi inayoendelewa kutekelezwa ambayo ni ya Sekta ya Afya, Maji na Elimu.

Miradi aliyoitembelea na kuikagua ni ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Maluga, mradi wa maji uliopo katika Kijiji cha Maluga ambao unagharimu zaidi Sh.424 Bilioni, ujenzi wa kituo cha Afya Kisiriri, ujenzi wa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na ujenzi wa Wodi ya dharura (EMD) katika Hospitali ya Wilaya ya Kiomboi na ujenzi wa Kituo cha Afya Kisiriri.

"Mkuu wa wilaya, mkurugenzi na timu yenu nawaombeni kamilisheni miradi hii yote iliyokuwa bado kukamilika  Serikali imetumia fedha nyingi kuitekeleza  kwa Mkoa wa Singida ni zaidi ya Sh.Bilioni 232 zimetolewa kwa ajili ya miradi mbalimbali" alisema Mahenge.

Aidha Mahenge alimuomba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kuhakikisha anapeleka miundombinu ya umeme, maji na barabara katika maeneo yote inapokamilishwa miradi hiyo ili iweze kufikiwa na wananchi kwa urahisi.

Alisema haiwezekani Serikali ikamilishe miradi mikubwa kwa fedha nyingi kiasi hicho lakini miundombinu ya maji, umeme na barabara isiwepo ambapo alimuomba mkurugenzi huyu kuhakikisha anakamilisha jambo hilo kwa haraka na wakati.

Dk.Mahenge alitumia nafasi hiyo kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwa kusimamia vizuri miradi hiyo na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo.

Akizungumzia miradi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda alisema miradi iliyotembelewa na Dk.Mahenge ni ujenzi wa  Kituo cha Afya Kisiriri ambao unatekelezwa kwa gharama ya Sh.250,000,000 na kuwa ujenzi wake upo katika hatua ya umaliziaji huku jengo la OPD likiwa kwenye hatua za upakaji wa rangi, kuwekwa milango na madirisha na halikadharika jengo la maabara.

Alitaja mradi mwingine kuwa ni ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Maluga ambao ujenzi wake utagharimu Sh.470 Milioni na ukamilisha wa ujenzi wa Wodi ya dharura (EMD) katika Hospitali ya Wilaya ambapo wamepokea Sh.300,000 ,000 na ujenzi wa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) unaotekelezwa kwa gharama ya Sh.250,000,000.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: