Na Mustafa Leu 

BAADA ya kupata teknolojia ya usanifu,ubunifu na utengebezajj wa zana za kisasa za kilimo,taasisi ya Imaratch,imejidhatiti kuleta mapinduzi makubwa kwenye kilimo kwa kuzalisha zana za kisasa za kilimo kulingana na mahitaji ya soko.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Imaratech, Alfred Chengura,anasema  taasidii hiyo imepata teknllojia hiyo ya utengenezaji wa zana za kisasa za kilimo kutoka Kituo cha uhamilishaji teknolojiavijijini CAMARTEC,ambayo  kimekuwa ni nguzo muhimu ya kutegemewa katika mapinduzi ya kilimo.

Anasema mafanikio hayo ya kusanifu,kubuni na kutengeza zana za kilimo yamepatikana kutokana na ufadhili  uliotolewa na Tume ya taifa ya Sayansi na teknolojia,COSTECH,Ufadhil ambao umeiwezesha Camartec kutoa teknolojia kwa taasisi hiyo ya Imaratech.


Teknolojia hiyo imeiwezesha Imaratech,kutengeza mashine mbalimbali na zana za kisasa ambazo zinatumika katika kilimo na kurahisisha uvunaji,kuongeza thamani ya mazao na imepata masoko ya kuuza zana hizo katika nchi za Kenya,Uganda,Rwanda,na Burundi

Chengura,anasema ,taasisi ya Imara Tech,inajivunia uwepo wa Camartec,ambayo ni kisima na hazina kubwa ya teknolijia ya usanifu,ubunifu na utengeneza  zana za kisasa za kilimo kwa lengo la kuleta mapinduzi makubwa kwenye kilimo

Chengura,anasema kuwa taasisi hiyo imekuwa ni kimbilio la wakulima kupata zana za kisasa na lengo ni kuhakikisha zana za kisasa zinawafikia wakulima wengi nchini ili waachane na matumizi ya jembe la mkono.



Anasisitiza matumizi ya  zana za kisasa za kilimo ambazo zita mkomboa mkulima ambapo atakuwa na uhakika wa kupata mazao mengi na hivyo kuongeza kipato cha familia

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: