NA. Majid Abdulkarim, MARA


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maswala ya Ukimwi, Kifua Kikuu, Madawa ya Kulevya  na Magonjwa yasiyoambukiza,  imewataka watanzania kujitokeza kupima afya zao katika vituo vya kutolea huduma za afya.


Rai hiyo imetolewa leo mkoani Mara na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Fatma Toufiq,  wakati kamati hiyo ilipotembelea Mgodi wa North Mara, ambapo ameutaka uongozi wa Mkoa kufanya  uhamasishaji kwa jamii ili kujitokeza kupima afya zao hali itakayowasaidia kuishi kwa malengo.


Mhe. Toufiq amesema kuwa, elimu ya uhamasishaji ya upimaji afya, ikitolewa kwa jamii  wakapata uelewa wa umuhimu wa kupima afya kutasaidia kujua afya zao na watakao gundulika kuwa na mambukizi wataanzishiwa dawa mara moja.


“Pima afya  Ishi kwa malengo, wasio pima wanaishi kwa matumaini maana yake hujui hali ya afya yako, jambo linalomfanya mtu kuishi na wasiwasi juu ya afya yake”, amesisitiza Mhe. Toufiq.


Mhe. Toufiq ameongeza kuwa, hakuna sababu ya kuogopa kupima afya yako kwa sababu dawa zipo, na kwamba iwapo utagundulika kuwa na maambukizi utaanzishiwa dawa.


Amewataka pia wataalamu wa afya nchini kuendelea kuhamasishana katika maeneo yao ya kazi, kujitokeza kupima afya zao ili kuleta ufanisi mzuri katika utendaji kazi wao kuliko kuishi kwa matumaini. 


“Wanaume mjitokeze kwa wingi kwenda kupima kwa sababu taaarfa zinaonyesha wanaume wengi mnategemea matokeo ya wanawake zenu na nyie hamjitokezi kupima afya zenu”, amesisitiza Mhe. Toufiq.


Aidha Mhe. Toufiq ameendelea kusema kuwa, mkoa huo unakila sababu ya kuendelea kutoa elimu kwa wale wanaoendelea kupata ujauzito kwenda kupima haraka na kujua afya zao  ili watoto watakao zaliwa wasiweze kupata maambukizi yoyote.


Ameeleza kuwa elimu ikitolewa mapema juu ya watu kujitokeza kupima afya zao, kutaongeza uwezekano wa kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi wakati wa wakuzaliwa kwa watoto.


Pia Mhe. Foufiq amezungumzia ugonjwa wa kifua kikuu, ambapo amesema, tunakila sababu ya kuhamasisha watu kujitokeza kupima ugonjwa huo, kwa kuwa dawa zipo na  unatibika

Share To:

Post A Comment: