Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Kalisti Lazaro amezindua rasmi zoezi la Anwani ya Makazi katika Halmashauri ya wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano Kwa viongozi watakaopita katika maeneo yao kwaajili ya zoezi hilo.

Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo lililofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto,Lazaro alisema kuwa Anwani za Makazi zitasaidia kutambua nyumba zote zilizopo Lushoto

Mkuu wa Wilaya huyo aliongeza kwa kusema kuwa zoezi hilo linatarajiwa kupita katika kata zote 33 ,Vijiji 125, vitongoji 943 na Kaya zaidi ya elfu 70 nakwamba zitatakiwa kupewa anwani za makazi ifikapo mwezi mei mwaka huu.

" Sisi wote tuliopo hapa tumepewa jukumu la kuhakikisha zoezi hili linatekelezwa katika maeneo yetu yote ikiwa ni pamoja na kutoa elimu Kwa wananchi ya nini maaana ya zoezi la anwani na faida zake" Alieleza Mkuu huyo wa Wilaya.

Aidha alisisitiza Kwa kuwataka wananchi kutoa ushirikiano Kwa timu ya watalaam ya anwani za Makazi ngazi ya Wilaya na timu za utekelezaji ngazi ya kata ,kamati za vijiji na watalaam mbalimbali ambao watakuwa wanapita kuwaomba taarifa zinazohusiana na operesheni hiyo.

" Uhamasishaji wa zoezi la Anwani za makazi kwa ngazi ya vijiji na vitongoji umefanyika kupitia Watendaji na tayari wameainisha barabara zilizopo na utoaji majina Kwa barabara zisizo na majina"Amesema Kalisti Lazaro

Lazaro alifafanua kuwa zoezi lililopo mbele yenu ni zoezi nyeti lenye hadhi ya kitaifa, na kwamba katika utekelezaji wake ninyi kama watumishi wa umma mliopewa dhamana hiyo mnao wajibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na kizingatia Sheria na kanuni.

Katika hatua nyingine amewataka Watendaji wa vijiji nao waunde timu za Utaratibu wa ngazi za kijiji na majina na timu ya hizo kuwasilishwa kwenye kata zenu na nakala Kwa timu ya uratibu ngazi za Wilaya .

Kufuatilia utekelezaji mfumo wa Anwani za makazi katika mitaa/vijiji / vitongoji Kwa kuhakikisha kwamba barabara /mitaa yote inatambuliwa inakuwa na majina,namba za nyumb zinaanishwa,mahitaji ya miundombinu yanaandaluwa taarifa za Anwani za makazi zinakusanywa na mfumo unawekwa

Mratibu wa Kamati ya Anwani ya Makazi wa Halmashauri hiyo Menard Mwimbile alisema kuwa tayari timu ya watu 12 wakiwemo Watendaji wa kata 33 na vijiji 125 wameshajengewa uwezo .

Mwenyekiti wa Halmashauri Mathew Mbarouk amesema zoezi hilo limekuja wakati muafaka licha ya kuchelewa kupata anwani hizo ambazo alisema zitarahisha mambo mengi.

Hata hivyo wananchi wa Wilaya hiyo wameipongeza serikali Kwa kuuamua kuja na zoezi la anwani za makazi nakwamba litasaidia kuondoa changamoto na usumbufu wa hapa na pale hasa Kwa wafanyabishara na wageni
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: