Baadhi ya wadau wa Maendeleo wilayani Mkalama wametoa msaada wa chakula kwenye Kambi ya watua wenye ulemavu ( wakoma) wanaoishi katika kijiji cha Nkungi kata ya Ilunda wilayani Mkalama.

Akikabidhi msaada kwaniaba ya wadau hao Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Sophia Kizigo amesema kuwa Serikali inawapenda na kuwajali watu wenye ulemavu hivyo itahakikisha inawawekea mazingira mazuri ya kuweza kupata chakula cha kutosha ili waweze kuendeleza maisha yao nakupatiwa haki za Msingi ikiwemo haki ya kuishi kama ilivyo kwa watu wengine.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwaalika wadau mbalimbali wa Maendeleo kujitokeza kusaidia watu wenye uhitaji kwani kwakufanya hivyo kutawafanya waishi maisha mazuri nakujiona wana umuhimu katika jamii.

Bw.Abel Kununta ni miongoni mwa watu wenye ulemavu wanaoishi kambini hapo alisema kuwa amefurahi kwa msaada wa chakula waliopatiwa na kuongeza kuwa viongozi wawe wanawatembelea kwa wakati ili waweze kujua afya zao kwani wamekua wakisumbulia na maradhi mbalimbali ambayo yasipotibiwa mapema yanapelekea wao kupoteza maisha.

Akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada huo Peter Sami ambaye ni mwenyekiti wa watu wenye ulemavu kambi ya Charedereko Nkungi ameshukuru kwa msaada huo na kuongeza kuwa chakula walichokipata leo kitawasaidia kwani kwa siku za hivi karibuni kumetokea ukosefu wa chakula Kwa wahitaji hao jambo lililowafanya wajisikie vibaya na kujihisi wametengwa na jamii.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: