Naibu Waziri wa Maji ambaye pia Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi ameendelea na kampeni yake ya kugawa majiko gas kwa wanawake lengo likiwa ni kupambana na uharinifu wa mazingira ili kulinda vyanzo vya maji.


Akiwa katika warsha ya siku mbili Jijjini Mbeya kupitia taasisi yake ya Maryprisca Women Foundation Empowerment Foundation(MWEF)amegawa majiko ya gas na mitungi yake kutoka kampuni ya Oryx kwa baadhi ya Kinamama   ntilie zaidi ya kumi waliofanya vizuri mahojiano.


Mahundi alisema wanawake ni watumiaji wakubwa wa nishati ya kuni na mkaa hivyo kwa kutumia majiko hayo watapunguza matumizi yanishati ya kuni na mkaa hivyo kulinda vyanzo vya maji ambavyo vinaharibiwa kutokana na ukataji miti.


Awali Taasisi ya MWEF hivi karibuni iligawa majiko mia tano hamsini bure na mitaji kwa baadhi ya wanawake kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya.


Naye mwalilishi wa kampuni ya Oryx gas alisema walitoa majiko zaidi ya mia tano kwa Mkurugenzi wa MWEF ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ili kuunga mkono juhudi za kupambana na uharibifu wa mazingira pia kulinda vyanzo vya maji hapa nchini na kwamba kampuni itatoa majiko mengine ili kuendeleza kampeni hiyo ambayo imeonesha kupata mwitikio mkubwa.

Share To:

Post A Comment: