Na Ahmed Mahmoud, WATU 1800 wanapata chanjo ya Uviko-19 Mkoani Tanga, kwa siku tofauti na awali ambapo idadi ilikuwa 500 kwa siku. Mganga mkuu wa mkoa wa Tanga, Dkt ,Jonathan Badem ameyasema hayo Jijini Tanga kwenye kikao cha kamati ya Uhamasishaji wa Chanjo ya kitaifa ofisini mwake walipofika kujitambulisha wakati akielezea sekta ya afya. Dkt Badem alisema hivi sasa kuna mwamko tofauti na awali walikuwa wanachanjwa watu 66 kwa siku ila hivi sasa wanachanjwa watu 500 kwa siku. “Ongezeko hilo la watu kuchanjwa limekuja baada ya kuingia chanjo mpya ya Sinopharm, ambapo watu wengi wameichangamkia,” alisema Dkt . Alisema walipokea dozi mpya 36,766 na hadi hivi sasa wamechanja watu 36,112 kwenye Wilaya sita za mkoa wa Tanga. Alisema mipango ya idara ya afya ni kuongeza kasi ya kuchanja hadi kufikia watu 3,000 hadi 4000 kwa siku. “Hali ikiendelea kuwa hivi itatuchukua muda wa miezi sita kufikia asilimia 60 ya malengo tuliyojiwekea,” amesema Dk Kayera. Alisema ushirikiano wa viongozi wa mkoa huo wa kisiasa, kidini na kimila ndiyo imekuwa chachu ya watu kuzidi kujitokeza kuchanja. “Nawasihi wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya Uviko-19 kwenye mahospitali, vituo vya afya na zahanati. Kwa Upande wake Mratibu wa Timu ya Taifa ya Uhamasishaji Regina alisema kuwa zoezi hilo linaendelea vizuri licha ya changamoto kadhaa walizokutana nazo katika vituo vya Afya katika maeneo kadhaa ya wilaya walipopita. Aliwataka wahudumu wa Afya kuendelea kuhamasisha chanjo ya Uviko 19 sanjari na Afua zingine za mapambano dhidi ya Korona ili kuendana na dhana nzima ya awamu ya pili ya uhamasishaji kwa kuwatumia wahudumu wa Afya Ngazi ya jamii. “Niwasihii sana watendaji wa Afya mliopewa dhamana hii ya upimaji wa chanjo ya Uviko 19 zoezi hili liendane na Afua zongine ikiwemo uvaaji wa Barakoa utumiaji wa maji tiririka bila kusahau kuwatumia wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kwani wanawajua wananchi na imethibitika kuwa ndio chachu ya kuongeza idadi ya wapimaji sanajri na viongozi wa serikali dini na mila”
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: