Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Beatus Choaji akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakaguzi wa Dawa na Vifaa Tiba wa Halmashauri za Mkoa wa Singida yalioanza leo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).
Kaimu Meneja wa Kanda ya Kati wa TMDA Sonia Mkumbwa akizungumzia suala zima la ukasimishaji wa baadhi ya madaraka na majukumu kwenye Halmashauri za wilaya.

Afisa Elimu kwa Umma na Huduma kwa Wateja TMDA Kanda ya Kati, Hussein Makame akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Mfamasia Mkuu wa Mkoa wa Singida,  Elikana Lubango akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mchunguzi wa dawa kutoka TMDA Kanda ya Kati, James Tanguye akizungumzia maadili na wajibu wa wakaguzi hao.
Mfamasia kutoka Singida DC, Mahagera Bupamba akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba Vicent Gyunda akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.

Mkaguzi wa Dawa wa TMDA kutoka Kanda ya Kati, Zakayo Kamani akijibu maswali ya washiriki wa mafunzo hayo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Philip Kitundu akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Maofisa wa TMDA wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mtaalamu wa Maabara, Pendo Kihula akielezea umuhimu wa mafunzo hayo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Ibrahim Pazia akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.


Na Dotto Mwaibale, Singida

 

WAKAGUZI wa Dawa na Vifaa Tiba wa Halmashauri za Mkoa wa Singida wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi na uzalendo ili kulinda afya za wananchi na waweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa. 

Ombi hilo limetolewa na mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Beatus Choaji wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakaguzi wa Dawa na Vifaa Tiba wa Halmashauri za Mkoa wa Singida yalioanza leo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) 

"Nitumie nafasi hii kuwashukuru TMDA kwa kujali afya za wananchi na kuamua kutoa mafunzo haya mkoani hapa na kukasimisha baadhi ya majukumu yenu ngazi ya halmashauri lengo likiwa ni kulinda afya za watanzania ili ni jambo zuri" alisema Choaji. 

Alisema TMDA  ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto yenye jukumu la kuthibiti ubora, usalama, ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi na kuwa imeundwa chini ya sheria ya dawa na vifaa tiba sura namba 219. 

Alisema majukuku ya TMDA ndiyo yanayo paswa kufanywa na wakaguzi hao hivyo ni jukumu lao  kuyalinda na si ya kuyapuuzia kwa kuwa wanafanya kazi ya kulinda afya za wananchi wa Tanzania. 

Kaimu Meneja wa Kanda ya Kati  TMDA Sonia Mkumbwa akizungumzia suala zima la ukasimishaji wa baadhi ya madaraka na majukumu kwenye halmashauri alisema kulitokana na mamlaka aliyopewa Waziri mwenye dhamana ya Afya chini ya Kifungu cha 121 cha Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba, Sura 219. 

"TMDA imekasimisha majukumu yake kupitia Kanuni za Kukasimu baadhi ya Madaraka na Majukumu ya TMDA kwa Halmashauri kupitia GN No. 476 za Mwaka 2015 pamoja na marekebisho yake GN No. 19 ya mwaka 2017" alisema Mkumbwa. 

Alisema katika kukasimu majukumu na madaraka hayo, Waziri amezingatia pia kifungu cha 113(2) cha Sheria ya Serikali za Mitaa ya Halmashauri za Wilaya [Local Government (District Authorities) Act], Sura 287 na kifungu cha 57(2) cha Sheria ya Serikali za Mitaa ya Halmashauri za Miji [Local Government (Urban Authorities) Act), Sura 288. 

Aliongeza kuwa lengo kuu la kukasimisha baadhi ya madaraka na majukumu ya TMDA kwa Halmashauri ni kusogeza karibu na wananchi huduma za udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi. 

Mchunguzi wa dawa kutoka TMDA James Tanguye akizungumzia maadili na wajibu wa wakaguzi hao alisema wanapaswa kuzingatia Utaalam (Professionalism),Uaminifu na kutimiza wajibu. 

Alisema malengo ya mafunzo hayo kwa wakaguzi hao ni kuongeza uelewa wa wakaguzi kuhusu maadili na wajibu wa wakaguzi kusisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili na kuwakumbusha kufanya kazi kwa ueledi na kutoa maamuzi sahihi kulingana na Sheria na taratibu za kazi na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.


Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: