Sunday, 19 December 2021

Mkoa wa Pwani una Uhaba wa magari ya wagonjwa 18.

 


Julieth Ngarabali.   Chalinze. 


Mkoa wa Pwani una uhaba wa magari ya kubebea wagonjwa  18  changamoto ambayo inachangia adha ya usafi kwa wagonjwa hasa wale wa rufaa kutoka katika kituo kimoja kwenda kingine.


Mkuu wa mkoa wa Pwani    Abubakar Kunenge amesema mkoa huo unahitaji kuwa na  magari ya wagonjwa  38 lakini kwa Sasa yaliyopo ni 22 ambapo kati yake mawili ni mabovu .


Kunenge amesema hayo Desemba 17 alipokua akikabidhi gari moja la wagonjwa  (ambulance) litakalotoa huduma katika kituo Cha Afya Kibindu ambacho kipi umbali wa kilomita 126 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Chalinze.


Gari hilo ni la aina ya Landcruiser na kwamba limenunuliwa kwa sh. Mil. 120 fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.


Mkuu huyo  wa mkoa ameipongeza Chalinze kwa kununua gari Hilo kwa mapato yake ya ndani na kubainisha kuwa sababu kubwa ya Serikali kuzianzisha Halmashauri pamoja na kurudisha maamuzi kwa wananchi wenyewe kusogeza huduma kwa jamii ni pamoja na kusaidia Seriakki kutoka huduma.


"Zinatakiwa kila Halmashauri zijiendeshe wenyewe,Sasa kujiendesha ndio Kama haya mnayofanya na mmesema wenyewe kila mwaka mmepanga kupata gari moja  na mkiwa na vipaumbele sahihi mnaweza"amesema  Kunenge.


Kunenge amesema kwa kupitia mfano huo wa Chalinze ametoa agizo kwa katibu tawala mkoa, wakurugenzi Halmashauri zote Tisa ziweke utaratibu wa kupata magari hayo ya kuhudumia wagonjwa  na kuweka miundombinu   ya kupata nyumba za watumishi wa idara hiyo.


Aidha magari hayo yawe yanafanyiwa matengenezo Kama ambavyo  utaalamu unataka kwa sababu yakiachwa baada ya muda yanachakaa na kuharibika.


"Na magari haya yanatumika unaona kwanza yanaenda kwa Kasi mwendo wake ni wa haraka  na ni magari yanayotumika wakati wa dharura na kwa muundo wetu tuna vituo vya afya,zahanati, hospital za wilaya na mpaka za Rufaa za mkoa na Taifa na hii inatokana na aina ya changamoto atakayokutana nayo mwananchi kwa upande wa afya hivyo nii lazima tuwe na magari haya, hivyo nawapongeza Sana Chalinze"amesema


Awali akitoa taarifa ya manunuzi ya gari hilo kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Chalinze  Ramdhani Possi,Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dr. Allen Mlekwa ameeleza kuwa kwa kipindi cha robo ya Julai hadi Septemba mwaka huu Takwimu za wagonjwa aa rufaa ilikua watu 90.


Dr. Mlekwa amesema huduma ya magari ya wagonjwa ni muhimu kwa sababu ya uwepo wa wagonjwa wa rufaa wanaotokana na matatizo mbalimbali ya uzazi ,ajali za barabarani, mahitaji ya damu na matatizo memgine na kwamba gari hilo litahudumia pia kata zingine za Mbwewe na Kimange


 Diwani wa kata ya Kibindu  Ramadhan Mkufya amesema  gari hilo itakwenda kupunguza adha na hata vifo vya watoto wadogo na wajawazito kwa sababu Sasa uhakika wa kupata usafiri wa rufaa kwa wakati tofauti na awali walikua wakitumia usafiri wa machela, baiskeli na pikipiki .


Mwakilishi wa  wananchi wa Kata ya Kibindu  Amina Almasi ameishukuru Halmashauri hiyo kuwapa usafiri wa uhaka  kwa sababu imewaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu zaidi ya kilomita 40 kwenda kufata huduma kituo jirani.

No comments:

Post a Comment