Na Pamela Mollel,Mkomazi


Hifadhi ya Taifa Mkomazi imepewa jukumu la kuzalisha wanyama jamii ya Faru ambao wapo hatarini kutoweka Duniani

Mradi huo wa kuzalisha faru weusi ulianza rasmi 1997 ambapo serikali ilianza juhudi za kurudisha maeneo ambayo kiasili wanyama hao walikuwa wakipatikana

Mtaalam wa Faru na mwendesha watalii katika hifadhi hiyo Edward Kimaro alisema kuwa 1985 faru weusi walipotea kabisa hali iliyopelekea mradi huo kuanza kwa kuleta faru 4 kutoka Afrika ya kusini mwaka 2001 wengine kutoka Ungereza, 2012 waliletwa kutoka Ulaya

Alisema faru hao walikuwa katika mradi wa uzaliano na kwa muda huo hazikuruhusiwa shughuli za utalii

"Mwaka 2017 hadi 2018 mahitaji ya utalii yaliongezeka ambapo watalii waliokuja katika hifadhi hiyo walitamani kuona faru na ndipo walitolewa faru 6 kwenye mradi ili kufanikisha Utalii wa faru"alisema Kimaro

Mtaalum huyo wa faru aliongeza kuwa wanyama hao ni adimu sana kuonekana ambapo Jumuiya za kimataifa katika uhifadhi wa viumbe hai duniani imewaweka katika kundi la wanyama waliopo hatarini kutoweka na kwa sababu hizo kila Taifa linafanya juhudi mbalimbali za kuwaweka hai kwa manufaa ya kizazi kijacho

"Historia katika hifadhi hii inasema kuwa 1970 walikuwepo faru weusi elfu kumi(10,000)ndani ya hifadhi kwa nchi nzima,1985 walipotea kutokana na ujangili na ndani ya miaka kumi baadae Tanzania ilikuwa na faru chini ya 200"alisema Kimaro

Mhifadhi mwandamizi hifadhi ya Mkomazi Happiness Kiemi alisema kuelekea miaka 60 ya Uhuru hifadhi hiyo imeboreshwa ikiwemo miundombinu ya barabara inayomuezesha mtalii yeyote kufika kiuraisi katika eneo hilo

"Hifadhi yetu ni kati ya hifadhi rahisi sana kufikika na ni sehemu ambayo unawezakuona wanyama kwa urahisi"alisema Kiemi

Katika kuchochea utalii hifadhi hiyo imeanzisha utalii wa usiku ambapo watalii wanaolala hifadhini hapo wanapata fursa ya kuona wanyama wanaoonekana usiku tu

Hata hivyo hifadhi hiyo ipo mbioni kuanzisha utalii wa mikutano ikiwemo kujenga kumbi mbalimbali kwaajili ya utalii wa mikutano

"Naomba niwakaribishe wadau wa utalii kuja kuwekeza katika hifadhi hii kwa kujenga hoteli za kitalii zitakazo saidia kuchochea utalii na kuongeza pato la Taifa"alisema Kiemi
Mhifadhi mwandamizi hifadhi ya Mkomazi Happiness Kiemi akielezea hifadhi ya Mkomazi namna walivyoboresha kuelekea miaka 60 ya uhuru
Mtalii kutoka Poland Jan Sikorsi anaelezea namna alivyofurahia vivutio vinavyopatika Katika hifadhi ya Mkomazi
Faru mweusi anayepatikana katika hifadhi ya Mkomazi,Faru huyu ni matokeo ya mradi wa kuzalisha faru
Mtaalam wa faru na mwendesha watalii katika hifadhi ya Mkomazi Edward Kimaro akielezea mradi wa uzalishaji wa faru kwa waandishi wa habari waliofika hifadhini hapo hivi karibu

Share To:

Post A Comment: