Na Angela Msimbira IRINGA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mhe Ummy Mwalimu  amesema hatamuonea aibu Mkurugenzi  wa Halmashauri  ambaye hatatenga na kutoa  fedha kwa ajili  ya kuwawezesha wanawake  kiuchumi kwa kuwa wanawake ndo jeshi la mabadiliko nchini


Akifungua Kongamano la uwezeshaji wanawake kiuchumi na kijamii Mkoa wa Iringa leo  Waziri Ummy amesema  wananwake ndio wanaolea familia, wanasomesha  watoto na kufanya shughuli za maendeleo katika nchi yetu


Amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini  kutoa mikopo yenye tija  na mikopo itakayowawezesha  kuanzisha viwanda ,kuanzisha  biashara na mikopo itakayowezesha kuongeza ajira  kwa watu wengine, mambo ya kutoa mikopo kiduchu yamepitwa na wakati.


Amesema kuwa  maafisa  maendeleo ya jamii  wanajukumu  la kusimamia  na kutoa ushauri kwa vikundi vya akina mama ili waweze kutumia mikopo waliyopata kwa kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo katika jamii


Amesema wanawake na vijana wana mawazo mazuri ya kuanzisha biashara zao ila sasa wakipeleka maombi kwenye Halmashauri wanaambiwa na Halmashauri hawawezi kupatiwa mkopo hadi wawe na biashara,lakini  sheria ya fedha  za Serikali  za mitaa na kanuni  za usimamizi wa mikopo  kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu  zinaelekeza mikopo itolewe kwa madhumuni  mawili; ya kuwawezesha wanawake,vijana na watu wenye ulemavu  kuanzisha shughuli zao au kuendeleza shughuli zao


“Wananchi wamekuwa hawapewi mikopo kwa kigezo kuwa mikopo haitolewi kwa vikundi vinavyoanzisha  biashara, hii haina maana ya utoaji wa mikopo lengo ni kutoa mikopo kwa ajili ya kuwakwamua  kiuchumi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, hivyo ninawaagiza wakurugenzi wa Halmashauri kufuata sheria na taratibu za utoaji wa Mikopo nchini “ amesisitiza Waziri Ummy.


Amesema watu wanamawazo  mazuri ya biashara , wameandika maandiko mazuri ya biashara lakini hawana biashara wanaomba mikopo  wanaambiwa lazima na biashara au  sehemu za kufanyia biashara, ni kinyume na sheria na utaratibu  kwa kuwa kanuni zinasema mikopo itolewe  kwa ajili ya kuanzisha biashara au shughuli za ujasiriamali  na kuendeleza, hivyo ni ruksa kupata mkopo


Amewaelekeza Halmashauri kujiridhisha  na maandiko ya biashara yanayoletwa na wahusika kama yanarudisha fedha zilizoombwa na kazi hiyo inatakiwa kutekelezwa na maafisa maendeleo ya jamii,


Aidha, amezisitiza Halmashauri  kuacha kuweka vikwazo  katika suala zima la utoaji wa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kupunguza ukiritimba  na kuwazungusha wakopaji kwa kuwa kwa kufanya hivyo ni kurudisha  nyuma maendeleo ya Taifa

Share To:

Post A Comment: