Friday, 26 November 2021

WAZIRI MAHUNDI AWASILI SUDAN NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb) amewasili mji wa Juba, Jamhuri ya Sudan ya Kusini akiiwakilisha Tanzania katika kikao cha Baraza la Mawaziri kinachojumuisha Mawaziri wa nchi za Bonde la Mto Nile.


Kikao hicho ni kikao kazi, ikiwa ni mwendelezo wa kalenda ya vikao hivyo ambapo kikao cha awali kilifanyika Addis Abbaba nchini Ethiopia ambapo pia Naibu Waziri Mhandisi Mahundi aliiwakilisha Tanzania.


Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na kujengeana uwezo wa kitaalam juu ya kuhifadhi maji na utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ili kuondoa changamoto za maji mijini na vijijini katika nchi husika.


Baadhi ya nchi zinazonufaika na Bonde la Mto Nile ni pamoja na Tanzania,Uganda,Sudan,Ethiopia na Misri.

No comments:

Post a Comment