Na Joachim Nyambo,Mbeya.


 


CHAMA cha wakulima nchini(TFA) kimetakiwa kulisaidia taifa kuondokana na changamoto ya kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi kwa kuzalisha kwa wingi mazao ya mbegu zinazozalisha bidhaa hiyo.


 


TFA imetajwa kuwa chombo muhimu kinachoweza kulisaidia taifa kufikia malengo yake ya kutoagiza mafuta ya kula nje ya nchi kutokana na ukongwe wake katika utoaji huduma kwa wakulima ikiwemo kuwapa ushauri sambamba na kuwatafutia masoko.


 


Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alibainisha hayo kwenye hotuba yake iliyosomwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya,Juma Homera katika kufungua Mkutano mkuu wa wanahisa wa TFA uliofanyika jijini Mbeya.


 


Alisema dhamira ya serikali ni kutokuagiza mafuta nje ya nchi  hivyo TFA wanayo kazi kubwa kuhakikisha kwamba wanaungana na serikali kuhakikisha mafuta ya kutosha yanapatikana nchini na kuondokana na changamoto ya kuagiza kutoka nje.


 


Alipongeza uongozi wa TFA kwa kuonyesha ukomavu baada ya chama hicho kupitia changamoto kadhaa za kiutendaji lakini wakaendelea kubaki imara kwa kuanza kupata faida na kuimarisha mtandao wao wa pembejeo.


 


“Nikiri kuwa serikali ina taarifa za hayo yote na iko tayari kushirikiana  nanyi kuhakikisha wakulima wan chi hii wananufaika na uwepo wenu.Wananchi wote na wanachama wa TFA watumie vizuri mtandao huu kwani TFA inalenga kumwondoa mkulima kwenye changamoto za matumizi ya pembejeo hafifu za kilimo.”


 


Aliwahakikishia wakulima na wanachama wa TFA kuwa katika kulenga kuwaondolea wakulima changamoto ya matumizi ya  pembejeo hafifu serikali kupitia wizara ya kilimo imeweka mfumo ambao utasimamiwa na Taasisi ya udhibiti wa viuwatilifu kwaajili ya uhakiki wa ubora ujulikanao kama Tii hakiki ambaoutawezesha mkulimakujua iwapo kiuwatilifu hakika kimesajiriwa na serikali ya Tanzania kwa matumizi yake.


 


Nchemba alisema kumekuwa na changamoto kubwa ya uletwaji wa viuwatilifu ambavyo havina ubora na kuweza kuharibu hata udongo uliopo kwenye maeneo yetu na hata kuharibu uzalishaji  kwenye mazao hapa nchini.


 


Alisema TPRI wamepewa kazi hiyo muhimu kuhakikisha kunakuwa na viuwatilifu vilivyo na ubora ili kutoendelea kumsababishia hasara mkulima na kumfanya awe na uhakika kwenye uzalishaji.


 


Alipongeza pia hatua ya TFA kuwasilisha serikalini wazo la kutumia hekta 500 kwaajili ya kuzalisha mbegu mbalimbali zikiwemo za alizeti kwa kushirikiana na  serikali.


 


Alisema wazo hilo limekuja wakati muafaka ambapo serikali kupitia wizara ya kilimo katika bajeti yake imewekakipaumbele cha kuongeza uzalishaji wa  wa mbegu mbalimbali za mazao hapa nchini ili kupunguza gharama za pembejeo na kuongeza tija katika kilimo na hasa uzalishaji wa alizeti ili kuongeza uzalishaji wa mafuta nchini.


 


Alisema lengo la mpango huo ni kuipunguzia serikali gharama za uagizaji wa mafuta nje ya nchi ambao umekuwa ukigharimu zaidi ya Shilingi bilioni 443 za kitanzania kwa mwaka  sawa na dola za kimarekani milioni 189.3 alizosema ni gharama kubwa sana.


 


Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa TFA Justin Shirima alisema taasisi hiyo ilipata hasara kwa kipindi cha miongo mitatu mfululizo lakini hivi sasa imeimarika kkatika kipindi cha miaka mitano mfululizo na kuanza kutengeneza faida.


 


“Ni busara kusema kwamba tumetengeneza hasara kwa miaongo zaidi ya mitatu na sasa kwa miaka mitano mfululizo tunatengeneza faida.Lakini kutengeneza faida pekee hakutoshi..niwa kati huu ambao sasa tunakuja na bidhaa nyingi mbadala..Utaona kipindi hiki cha mbolea janga kubwa la Corona lilivyotokea duniani kumekuwa na tatizo la uzalishaji wa mbolea kwa nchi tunazoagiza..sisi tumefanya juhudi tumeleta mbolea mbadala inaitwa TFA Fahari.” Alisema


 


Shirima alisema lengo la kuzalisha TFA Fahari ni kupungtuza changamoto ya upatikanaji wa mbolea nchini huku pia ikisimamia upatikanaji wa viuwatilifu vilivyohakikiwa ambavyo ni salama kwa matumizi ya kilimo.


 



Share To:

Post A Comment: