Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeendesha semina elekezi ya kuwajengea uwezo Wahariri wa Vyombo vya Habari, Waandishi na Washawishi wa Mitandao ya Kijamii kuhusu Mfumo wa malipo ya Maegesho kwa njia ya Kielektroniki (TeRMIS) unaotarajiwa kuanza kutumika tarehe 1 Desemba, 2021 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Singida na Mwanza.


Mtumiaji wa Maegesho anapaswa kulipia Ushuru wa Maegesho Kidigitali baada ya kupatiwa namba ya malipo (control number) ambapo atatumia Kumbukumbu namba hiyo kulipia maegesho kwa kutumia mtandao wowote wa simu ya mkononi, Benki ya NMB na CRDB au kupitia kwa Mawakala wa Huduma za fedha.

Mfumo huu wa Kidigitali unampa muda mtumiaji wa maegesho kulipia Ushuru wa Maegesho ndani ya Siku 14 tangu alipotumia Maegesho na endapo atashindwa kulipa ndani ya muda huo atatakiwa kulipa Ushuru wa Maegesho pamoja na faini ya Shilingi 10,000/=.

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam, mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 500 kwa Saa na Shilingi 2,500 kwa Siku.

Mkoa wa Mwanza mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 500 kwa Saa na Shilingi 1,500 kwa Siku.

Mkoa wa Iringa mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 300 kwa Saa na Shilingi 1,000 kwa Siku.

Mkoa wa Dodoma mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 300 kwa Saa na Shilingi 1,000 kwa Siku.

Mkoa wa Singida mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 300 kwa Saa na Shilingi 1,000 kwa Siku.
Share To:

Post A Comment: