Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Kafulila Novemba 11,2021 amewapongeza wakurugenzi na wakuu wa wilaya tano za Mkoa wa Simiyu kwa kuendelea kuboresha usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Amesema ni juhudi hizo zilizofanikisha Mkoa wa Simiyu kushika nafasi ya nne mwaka huu 2021 kutoka nafasi ya 20 mwaka 2020.

"Mimi naona fahari kuwa na timu hii ya wakuu wa wilaya na wakurugenzi. Mbali ya kupaisha mkoa huu kutoka nafasi ya pili mkiani mwaka 2020 mpaka nafasi ya pili juu katika makusanyo ya halmashauri kimkoa, leo nimepata taarifa kuwa mkoa wetu umeshika nafasi ya nne kitaifa katika miradi ya Mwenge iliyokaguliwa kulinganisha na nafasi ya 20 mwaka 2020.

"Ninaamini mwakani tutashika nafasi ya kwanza.Angalia hapa Busega, taarifa ya makusanyo ya robo ya mwaka wa fedha 2020 ilikuwa asilimia 15 ya lengo kulinganisha na asilimia 29 kwenye robo ya kwanza mwaka 2021. Hivyo inawezekana. Tuendelee kupambana kujenga mkoa wetu," alisisitiza Kafulila katika hotuba yake kwenye Baraza la Madiwani wilaya ya Busega.

Share To:

Post A Comment: