Saturday, 27 November 2021

PICHA 30 : UZINDUZI WA KAMPENI JIMBO LA NGORONGORO

 


Katibu wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi, Mlezi wa Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Ndg. Shaka Hamdu Shaka  Amezindua Rasmi Kampeni za Uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ngorongoro na Kumnadi mgombea Ubunge jimbo la Ngorongoro kupitia Chama Cha Mapinduzi Ndg Emmanuel Shangai

Shaka amewaomba wakazi wa Tarafa ya Sale wilayani Ngorongoro, kumchagua mgombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo ili kuwaletea maendeleo yaliyoanza kuletwa na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwemo utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Loliondo mpaka Sale kwa kiwango cha lami kwa hatua ya kwanza,Ujenzi wa kituo cha Afya Sale sambamba na madarasa. 
 

Kwa upande wake mgombe wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo, Emmanuel Shangai , ameahidi kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi, {CCM} katika kuleta maendeleo kwa wananchi.

Aidha Ndg. Shaka aliongozana na viongozi mbalimbali wa Chama kutoka Makao Makuu ya CCM Taifa wakiongozwa na Katibu wa Nec, Idara ya Organaizeshen Dkt. Maudline Castico Uwanja wa Malambo, Kata ya Malambo, Tarafa ya Sale
No comments:

Post a Comment