Jane Edward, Arusha


Wadau wa matumizi ya Tehama kutoka nchi mbalimbali wamekutana jijini Arusha kwa lengo la kujadili mustakabali wa matumizi ya Tehama huku changamoto kubwa ikionyesha matumizi ya Tehama kukua kwa kiasi kikubwa huku vijana wakiwa ndiyo watumiaji wakubwa wa mitandao hiyo.


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha katika mkutano wa  tano wa mwaka wa Tehama Tanzania  uliowashirikisha wadau mbalimbali wa Tehama, Mkurugenzi wa Tehama wa wizara ya habari, mawasiliano na ateknolojia ya  habari,ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya mkutano huo,Mulembwa Munaku, amesema kuwa jamii ina wajibu wa kuhakikisha vijana wanatumia Tehama kwa matumizi sahihi na sio kupotosha umma .Ameongeza kuwa, hapa nchini asilimia 75 ya vijana wanatumia matumizi ya Tehama  kwa namna mbalimbali ikiwemo kudhihaki baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea kadhia kwenye familia ,hivyo amewataka vijana kutumia Tehama katika kuvumbua vitu mbalimbali vitakavyo wapatia ajira.


"Naomna niwaombe wazazi pamoja na walezi  kuwa  wana wajibu na jukumu kubwa la kuhakikisha tunawajengea msingi ulio bora vijana wetu  na kuhakikisha wanakuwa na matumizi sahihi ya Tehama katika kujiketea maendeleo."amesema 

 


Amefafanua zaidi  kuwa ,wizara ya habari inajikita zaidi katika kutoa elimu kwa vijana na jamii kutumia Tehama kama fursa na kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja. 


 Hata hivyo siku ya Ijumaa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kufungua mkutano huo wa tano wa wadau wa matumizi ya tehama.

Share To:

Post A Comment: