Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameshiriki kwenye hafla maalumu ya kukabidhiwa mitaji  zaidi ya Sh Mil 200 kwa vikundi 10 vya Wajasiriamali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na kuwataka kuelekeza mikopo waliyopata kwenye mitaji.


Mhandisi Maryprisca amesema Mheshimiwa Rais Mama Samia anapenda kuona wananchi wanapata unafuu wa maisha kwa kupatiwa mitaji isiyo na riba ili iwainue kiuchumi.


Amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuielekeza kwenye malengo yaliyokusudiwa ili kuweza kurejesha kwa urahisi na kufungua wigo kwa wengine kupata mikopo.


"Hakikisheni mikopo mliyopewa isiwagawanye,Kopa kwa Busara lipa kwa Wakati,Mikopo mliyopewa ikawaunganishe na kuwapa mafanikio baada ya kuzalisha faida"amesema Mhandisi Maryprisca.


Amebainisha kuwa mikopo hii isiyo na riba ni matunda ya Rais Samia Suluhu Hassan ambayo itaenda kuimarisha uchumi na kubadilisha mifumo ya maisha ikiwa ni pamoja na kupatiwa elimu ya namna bora ya kutumia mikopo hiyo.


Aidha Mhandisi Maryprisca ametumia fursa hiyo kuelezea namna ambavyo Wizara ya Maji inavyoendelea kuimarisha mifumo ya maji kwa kukarabati miundo mbinu chakavu ili huduma ya maji isogezwe karibu na makazi ya watu.


Amesema kuwa kupitia tozo za miamala ya simu Rais Samia ameongeza Mamilioni ya Fedha kwa ajili ya huduma za maji ili kuhakikisha tatizo la maji linamalizika.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: