Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani kulia akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati akitoa taarifa kwa Umma Juu ya uwepo wa upungufu wa upatikanaji wa Huduma ya Maji Safi kwa Wakazi wa Jiji la Tanga kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Rogers
Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani kulia akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati akitoa taarifa kwa Umma Juu ya uwepo wa upungufu wa upatikanaji wa Huduma ya Maji Safi kwa Wakazi wa Jiji la Tanga kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Rogers
AFISA Uhusiano wa Tanga Uwasa Dovetha Mayala akisisitiza jambo
Sehemu ya waandishi wa Habari wakifuatilia matukioo mbalimbali kwenye mkutano huo
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga
Uwasa) imeeleza sababu za kuanza kwa mgao wa maji katika Jiji la Tanga kwamba
inatokanana na kiasi kilichopo cha maji yanayozalishwa kiweze kusambazwa na kupatikana
kwa watu wote .
Hivyo kusababisha uwepo kwa upungufu mkubwa wa maji
katika maeneo ya Jiji la Tanga lenye wakazi wapatao 316,055 Tangu mwishoni mwa
mwezi Septemba 2021.
Mgao huo unatarajiwa kuanza Octoba 9 mwaka huu katika
maeneo ya Nguvumali,Kisosora,Mwamboni,Chumbageni,Kwaminchi,Chuda,Gofu,Ngamiani,Central,Bombo,Raskazone,Sahare,Usagara
na Makorora.
Maeneo mengine yatakayoathirika na mgao huo ni Duga, Magomeni,
Mabawa, Mwakizaro,Msambweni,Donge,Magaoni,TangaSisi,Mwang’ombe,Mwakidila,Mwahako,Masiwani,Mbugani,Machui,Tongoni,Kiwavu,Maere,Kivindani,Mtakuja
na Kange Kasera.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kaimu Mkurugenzi
wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani ambapo alisema hilo linatokana na kwa
kuzingatia majira ya mwaka Jijini Tanga ambapo kipindi cha kiangazi huanza
mwezi Agosti hadi Novemba kila mwaka.
Alisema ambapo kipindi hicho matumizi ya maji huongezeka
na hivyo kujitokeza kwa upungufu wa maji maeneo mengi kutokana na maji
yanayozalishwa kutokukudhi mahitaji ya maji kwa watu wote Jijini Tanga kwa
kipindi hicho.
“Upungufu huu unatokana na ukomo wa uzalishaji maji wa
mtambo wa kusafisha na kutibu maji Mowe kwani uwezo wa kuzalisha na kusambaza
maji ni wastani mita za ujazo 30000 kwa siku wakati mahitaji ya maji wakati wa
kiangazi yanakadiriwa kufikia wastani wa mita za ujazo 37100 kwa siku.
Alisema mgao huo umezingatia uwepo wa maeneo mengine
yenye ofisi za Umma,Vituo vya Afya ,Hospitali pamoja na taasisi za elimu ambako
muda mwingi wa mchana huduma ya maji inabidi iwepo.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi huyo ambaye pia ni Meneja
Ufundi wa Tanga Uwasa alisema kufuatia changamoto hiyo Rais Samia Suluhu pamoja
na jitihada za Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu na ufuatiliaji makini wa
karibu wa Waziri wa Maji Jumaa Aweso.
Alisema jitihada
hizo zimeiwezesha Tanga Uwasa kupata fedha kiasi cha Sh.Bilioni 9.8 ili kutekeleza mradi mkubwa unaolenga kuongeza
uwezo wa uzalishaji na usambazaji wa maji kutoka mita za ujazo 30,000 hadi 45,000
kwa siku ambapo ujenzi wa mradi huo ulianza mwezi Agosti mwaka huu na
unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti 2022.
Post A Comment: