Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Selemani Jafo akizungumza na baadhi ya Watendaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Waandishi wa Habari.

 

Serikali ya Tanzania imepiga marufuku utengenezaji na uwekaji wa Plastiki laini kwenye mifuniko ya chupa za maji (viremba vya juu) ikiwa pamoja na mirija ya Plastiki inayotumika katika vivywaji hivyo, katika kipindi cha miezi sita baada ya katazo hilo kuanzia Oktoba 11, 2021.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Selemani Jafo amesema katazo hilo limekuja baada ya kuwepo kwa athari za mazingira kwenye mazalia ya Samaki, Wanyama mbalimbali kutokana na Plastiki hizo kuenea kwenye nyasi, mifereji na vyanzo vingine vya Maji.

Jafo amesema kulingana na Kifungu cha Sheria ya nchi No. 13(2), Sheria No. 20 ya Sheria ya Mazingira, 2004 ametoa maelekezo ya kupiga marufuku hiyo ya kuweka Plastiki laini kwenye bidhaa hizo hapa nchini na bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi.

“Baada ya miezi Sita hatutarajii kuona bidhaa hizo zinazalishwa zikiwa na karatasi laini juu ya mifuniko, lazima tulinde mazingira yetu yanayotuzunguka”, amesema Jafo.

Amesema baada ya miezi Sita kuisha, Wazalishaji na Wasambazaji wa bidhaa hizo wanaelekezwa kuzalisha bidhaa zao bila kuweka Plastiki laini nje ya Chupa hizo.

 

Share To:

Post A Comment: