Friday, 8 October 2021

Serikali inatambua mchango wa wahariri ,vyombo vya habari uelimishaji Chanjo ya UVIKO-19-Msigwa

 


Na.Catherine Sungura,WAMJW-DSM 


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amewapongeza wahariri na vyombo vya habari nchini kwa jitihada  wanazofanya Katika kuhabarisha Umma juu ya chanjo ya UVIKO-19.


Msigwa ameyasema hayo Leo wakati wa warsha ya wahariri wa vyombo vya habari iliyofanyika Leo  jijini Dar es salaam.


Amesema kuwa katika kipindi Cha wiki mbili wahariri hao pamoja na vyombo vyao vya habari wameweza kufanya juhudi kubwa na kwa wiki mbili matunda yameonekana


"Kazi kubwa ambayo imefanywa na wahariri na vyombo vyao imesaidia kwa kiasi kikubwa ,niwapongeze sana kwani matokeo tunayaona".Aliwapongeza


Hata hivyo Msigwa ametoa wito kwa wananchi ambao hawajaweza kuchanjwa wajitokeze kwani takwimu zinaonesha wale ambao hawajachanjwa ndio wanaokuwa Kwenye Hali mbaya mara wapatapo MAAMBUKIZI ya UVIKO-19.


Naye, Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi kitengo Cha elimu ya afya kutoka Wizara ya Afya Dkt.Amalberga Kasangala amesema kuwa suala la kuelimisha ni mtambuka na hivyo inahitaji wataalam mbalimbali Katika kuwaelimisha wananchi.


"Katika kufanikisha hili wizara inashirikiana na Taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na wadau wengine wa Maendeleo  na kuhakikisha chanjo zote zinazoingia hapa nchini Zina usalama.


Dkt.Amaberga amesema kuwa Wanahabari wapo Katika hatari ya kupata maambukizi kulingana na mazingira wakati wa  utekelezaji wa majukumu yao hata hivyo amewataka wahakikishe wanaendekea kuwaelimisha wananchi kupata chanjo na wao wanachukua kinga ikiwa ni pamoja na kupata chanjo hiyo.

No comments:

Post a Comment