Wednesday, 20 October 2021

Prof. Shemdoe: Zingatieni nidhamu kwenye michezo

 


Na Asila Twaha- OR -TAMISEMI


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amewaagiza washiriki wa michezo  ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI kufuata sheria, taratibu za utumishi wa umma kuzingatia maadili katika kipindi chote cha mashindano ili kupata ushindi uliotukuka.


Prof. Shemdoe alitoa agizo hilo  Oktoba 18, 2021 Jijini Dodoma na kuwataka timu zote za Ofisi ya Rais - TAMISEMI  kuhakikisha inacheza kwa kujituma, bidii na nidhamu ili irudi na ushindi wa kishindo katika michezo yote itakayoshiriki. 


 “Nina imani  na sina wasiwasi  na mashindano hayo mnayoenda pia tuna uwakilishi mzuri  wa timu ya netball na juzi tu wa mekuja na Kombe la Nyerere CUP ambalo tumechukua ushindi wa Kitaifa” alisema Prof. Shemdoe.


Amesema kuwa  michezo ya SHIMIWI ni muhimu kwa sababu kwa kuwa inawakutanisha taasisi na Wizara za Serikali zote na inasaidia kuboresha afya na kuongeza hamasa ya utendaji kazi hivyo kuongeza tija na ufanisi wa kazi.


Alisisitiza kwa kuwataka wachezaji hao kuzingatia nidhamu katika michezo na maisha watakayokwenda kuishi kwa kipindi chote watakacho kuwa huko kwenye michezo kwa kujilinda na kujitunza kwani kuna mangonjwa. 


Naye Mkurugenzi wa Utawala za Rasilimali watu Victor Kategere amesema jumla ya washiriki 60 wanategemewa kushiriki michezo hiyo ambao watashiriki katika riadha, kuvuta kamba, mpira wa kikapu na Mpira wa Miguu na kusisitiza kuwa washiriki wote wapo vizuri kwa ushiriki. 


Kwa upande wake Katibu wa Tamisemi Sports Club Bwana Alex Moris ameahidi kurudi na ushindi kwa kuwa timu imejiandaa vizuri na ipo tayari kwa kwenda kushindana na kurudi na ushindi. 


Mashindano ya SHIMIWI mwaka huu yanafanyika Mkoani Morogoro na yanatarijiwa kufunguliwa tarehe 20/10/2021 na Makamu wa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Isdor Mpango

No comments:

Post a Comment