Hifadhi ya Taifa ya Arusha inahusisha Mlima Meru, mlima maarufu wa volcano wenye urefu wa meta 4566 (futi 14,977 au kilometa 4.6) kutoka usawa wa bahari, na ipo katika Mkoa wa Arusha, kaskazini mashariki mwa Tanzania.


Hifadhi hii ni ndogo iliyoanzishwa rasmi mwaka 1960, ikiwa na eneo la kilometa za mraba 137 tu, inavutia ikiwa na aina tofauti ya uoto katika maeneo matatu. Magharibi, Kasoko ya Meru (Meru Crater) kuna Mto Jekukumia; kilele cha Mlima Meru kinapatikana hapa.

 Kasoko ya Ngurdoto (Ngurdoto Crater) upande wa kusini-mashariki ni eneo la nyasi nyingi. Maziwa madogo yenye vina vifupi ya Momella yaliyojaa magadi kaskazini mashariki mwa hifadhi hii yanatofautiana kwa rangi na ni maarufu kwa aina nyingi za ndege wanaopatikana huko.
















































Share To:

Post A Comment: