Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ameendelelea na ziara  Mkoani Morogoro kwa  lengo la kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na Wizara mkoani hapo.


Akiwa katika kikao ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Mahundi amesema viongozi waandamizi wa Wizara hiyo wakiongozwa na Waziri Mhe. Jumaa Aweso, 

Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga pamoja na viongozi wengine wametawanyika mikoani ili kuhakikisha dhamira ya Mhe. Rais ya kumtua mama ndoo ya maji inafanikiwa hasa katika suala la  kuhakikisha fedha zote zilizotengwa zinatumika kama zilivyokusudiwa.


Kwa upande Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mariam Ntunguja amesema hali ya upatikanaji wa maji mkoani Morogoro hairidhirishi hasa kutokana na hali ya ukame unaendelea sehemu mbalimbali nchini.Aidha ameishukuru Wizara ya Maji kwa jinsi inavyotekeleza miradi ya maji Mkoani Morogoro.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando amemuomba Naibu Waziri wa Maji kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya mkoa wa Morogoro zinaletwa kwa wakati ili kuharakisha utekelezwaji wa miradi.

Share To:

Post A Comment: