Na mwandishi wetu,MbeyaMBUNGE wa vitimaalum Mkoa wa mbeya na Naibu waziri wa maji Mhandisi Maryprisca Mahundi  ameungana na baadhi ya Wananchi pamoja na Viongozi wa Kiserikali katika tukio la kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini Benson Mpesya aliyefariki Dunia Octoba 23, 2021.


Mhandisi Mahundi amesema kuwa mpesya ameacha pengo kubwa katika mkoa wa mbeya .


"Lakini pia marehemu Mpesya enzi za uhai wake alikuwa makamu mwenyekiti wa bodi ya maji ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jijini Mbeya ,kufuatia kifo hiki mamlaka tumepata pengo kubwa sana.kwani tumepoteza mtu mubinu "amesema Naibu waziri wa maji Mhandisi Mahundi.

Share To:

Post A Comment: