Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb)anaendelea na ziara zake za kutembelea vyanzo vya maji pia kutambulisha mabonde tisa nchini.


Akitembelea mwekezaji wa Highlands Estates Mahundi ameipongeza kampuni hiyo kwa kulinda chanzo na utunzaji wa mazingira.


Ameagiza uongozi wa Highlands Estates kujenga uzio kuzuia magari kupita eneo la chanzo kuzuia uharibifu wa mazingira sambamba na kuacha njia kwa watembea kwa miguu ili kuepusha mgongano.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbarali amesema jitihada zinazofanywa na serikali za kuhifadhi vyanzo vya maji zinakwamishwa na baadhi ya wafugaji kuiachia mifugo kiholela.


Aidha Fahad Pirmohamed Muller mwekezaji wa Highland Estates ameiomba mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji punguzo za tozo  za umeme kwani maji hayo mbali ya kampuni huwasaidia pia wananchi wengi wanaozunguka mfereji huo.

Share To:

Post A Comment: