Wednesday, 6 October 2021

MTAFITI WA KUTOKA TARI NALIENDELE ATAJA MAGONJWA YANAYOWATESA WAKULIMA WA ZAO LA KOROSHO NCHINI

MTAFITI kutoka Kituo cha Tari Naliendele Adadi Japhet Majun akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
MTAFITI kutoka Kituo cha Tari Naliendele Adadi Japhet Majun akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
Wakiwa kwenye picha ya Pamoja 


NA OSCAR ASSENGA, TANGA

MTAFITI kutoka Kituo cha Tari Naliniendele Adadili Japhet Majune ameyataja ugonjwa ambao umekuwa ukiwatesa wakulima wa zao Korosho nchini na usipozibitiwa unaweza kusababisha hasara ya asilimia 48 mpaka 100 kuwa ni ubiri unga.

Adadi aliyasema hayo leo wakati mafunzo ya siku ya pili yanayoendeshwa na bodi ya Korosho Tanzania kwa kushirikiana na Tari Naliendele ambayo yanashirikisha maafisa ugani na wapuliziaji wa viwatilifu katika mkoa wa Tanga .

Alisema kwamba iwapo ugonjwa huo utavamia shamba la mkulima wa zao hilo hawezi kupata chochote asipofanya upuliziaji wa haraka na badala yake atajikuta akipata hasara na hivyo kushindwa kupata manufaa.

“Lakini ugonjwa mwengine ni Braiti huu nao ni tatizo kwa wakulima wa korosho na lisipozibitiwa anaweza kupata hasara ya asilimia 48 mpaka 100 ya hasara “Alisema

Hata hivyo alisema ugonjwa mwengine ni Daybaki ambao unasabishwa na wadudu ambao wanaleta hasara kubwa wasipozibiti wanapata hasara kwa asilimia 50 wanaweza kupoteza mazao.

“Tupo Tanga kwa ajili ya kutoa mafunzo ya kilimo bora cha zao na korosho pamoja na matumizi sahihi ya viwatilifu pamoja na utambuzi wa magonjwa na wadudu waharibifu tumeona ugonjwa wa ubiri unga ni tatizo kubwa kwenye ukanda wa Tanga “Alisema

“Lakini bado wakulima hawajajua namna ya kuweza kuthibiti ugonjwa huu kwa hiyo tumewapa elimu na ninaamini baada ya mafunzo hayo wataweza kudhibti ugonjwa huo kwa lengo la waweze kupata mavuno ya kutosha”Alisema

Aidha Mtaalamu huyo alisema ugonjwa mwengine ambao ni hatari n wa braiti ambao ukianza kushambulia mazao hayo huwezi kuutofautisha magonjwa hayo lakini baada ya mafunzo hayo wameweza kuutofautisha.

Hata hivyo aliwaasa wakulima ili waweze kupata uzalishaji mzuri na bora lazima wahakikisha wanatumia viwatilifu kwa umakini na kuzingatia watalaamu wanachowashauri kwenye zao hilo la korosho.

Awali akizungumza Afisa Kilimo wa Bodi ya Korosho Tanzania Tanga Frank Mfutakamba alisema mafunzo hayo yanafanyika siku mbili kila kituo kwa mkoa wa Tanga lengo likiwa kuwajengea uwezo maafisa ugani na wapuliziaji .

“Kubwa ni juu ya kilimo bora cha korosha na upuliziaji wa viwatilifu na hii imetokana na kwamba misimu miwili iliyopita kulikuwa korosho ambazo hazina ubora”Alisema

Mwisho.

No comments:

Post a Comment