Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa kushirikiana na wananchi leo ameanzisha ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Mkoyo ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuboresha sekta ya Elimu katika Jimbo la Dodoma Mjini.


Mbunge Mavunde ameshiriki katika zoezi la uchimbaji msingi wa madarasa na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa Hombolo Mkoyo kwa kujitolea nguvukazi ili kufanikisha zoezi hilo ambapo Shule hii ikikamilika itawapunguzia mwendo wanafunzi wa Mkoyo wanaotembea kilomita  9 kufuata Shule ya Sekondari Hombolo Bwawani.


Katika kuanzisha mchakato wa ujenzi huo wa ujenzi wa madarasa kwa ajili ya Sekondari Mbunge Mavunde amechangia kokoto,saruji mifuko 100 na matofali 2000.

Aidha zoezi hilo lilitanguliwa na ukaguzi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Ngh’ole ambapo Mbunge Mavunde alichangia matofali 1000 na saruji mifuko 80 pamoja Shule Mpya ya Ndachi ambapo pia amechangia matofali 2000 na saruji mifuko 130.


Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa kata ya Hombolo Bwawani  Assed Ndajilo amemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo amekuwa chachu ya maendeleo katika kata ya Hombolo Bwawani na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano ili kukamilisha miradi yote aliyoianzisha.

Share To:

Post A Comment: