Katika milele Cha maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoani Arusha, Wanawake wa Umoja huo wamempongeza Mhe.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri wa Muungano na kumwahidi kumpa ushirikiano kwa kumuunga Mkono "UWT tunasema twende pamoja na Samia kwa haraka zaidi, Kazi inaendelea" amehimiza Jasmini  Bachu wenyekiti wa UWT Mkoa wa Arusha

Aidha, Jasmini amesema maadhimisho hayo Mkoani Arusha yamefanyika yana mafanikio makubwa kwani Wilaya zote zimeshiriki kuanzia ngazi ya Tawi ambapo Wanawake wameshiriki shughuli za kijamii kama vile kufanya Usafi kwenye masomo, vituo vya kutokea huduma za afya, vyanzo vya Maji pia Wanawake wameweza kuwatembelea na kutoa misaada kwa watu wasiojiweza.

Katika kuunga Mkono jitahada za Mhe.Rais kuitangaza utalii Wanawake hao wamekua na maonyesho ya bidhaaa za asili zinazovutia utalii sambamba na kuhamasisha uchukuaji tahadhari juu ya UVIKO-19  kwa kuhamasisha ulaji wa CHAKULA vyenye lishe

Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Ndg.Zolothe Steven Zolothe ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha amepongeza  Halmashauri za Mkoa wa Arusha kwa utoaji wa mikopo kwa vikundi vya Wanawake Vijana na Watu wenye ulemavu na kutoa wito kwa Halmashauri hizo kuongeza kasi ya utoaji wa mikopo hiyo Ili kuwawezesha Wanawake kujikwamua kiuchumi.

Pia Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kichama Meru Bi .Julieth Maturo amesema Wanawake ni Kesho kubwa na wapo tayari kushiriki kikamilifu kuijenga nchi.

Naye, Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi CCM Wilaya ya Kichama  Meru Bi.Angela Pallangyo ametoa wito kwa kina mama  kuendelea kutoa malezi bora kwa  watoto katika zama hizi zenye changamoto ya kuporomoka kwa maadili" tuige mfano kwa wazazi wetu Ili tuweze kuwa na kina mama na kina baba wa kesho wenye maadili" amehimiza Angela 

Katibu wa CCM Wilaya ya Kichama Meru Ndg.Gurisha Mfanga amesema Serekali Wilayani humo inashirikiana vyema na Chama katika utekelezaji wa ilani ya CCM ambapo amepongeza Uongozi wa Wilaya na Halmashauri.


Vilevile Mfango ametoa wito kwa Wanawake kuendelea kuchukua tahadhari juu ya Ugonjwa wa UVIKO-19 kwa kupata chanjo.


Share To:

Post A Comment: