Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.


Serikali imetoa rai  kwa wahandisi kote nchini kuendelea kujisajili chini ya bodi  ya  usajili wa Wahandisi Tanzania[ERB] ili waweze kutambulika kitaifa na kimataifa  .



Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma na katibu mkuu Wizara ya maji mhandisi Anthony Sanga katika hitimisho la mkutano wa 18 wa wahandisi nchini  uliokwenda sambamba na kalimbiu isemayo athari ya mapinduzi ya nne ya viwanda kwenye miundombinu.


Mhandisi Sanga amesema kwa kuwa kujisajili kwa wahandisi ni takwa la kisheria hivyo mlango uko wazi kwa kila mhandisi kujisajili huku akihimiza kwa wahitimu fani ya uhandisi kutoka vyuo mbalimbali kuchangamkia fursa hiyo.




Mhandisi Sanga amesema kufanya hivyo itasaidia zaidi wahandisi kuaminika kitaifa na kimataifa zaidi pamoja na kuepusha watu wanaofanya kazi ya uhandisi kutekeleza miradi ya miundombinu licha ya kuwa hawana vigezo hali ambayo husababisha miradi kutekelezwa kwa kiwango cha chini.


Msajili wa bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania [ERB]Mhandisi Patrick Barozi amesema katika mkutano huo  wa siku tatu kulihusishwa mjadala wa kitaaluma,maonesho ya ubunifu,sayansi na teknolojia huku pia makampuni 61 yakishiriki.



Mwenyekiti wa bodi ya Wahandisi Tanzania[ERB]Mhandisi Prof.Ninatubu Lema amesema katika mkutano huo zaidi ya watu  800 wamefuatilia kwa njia ya mtandao hivyo idadi ya watu wote waliofuatilia ikiwa  ni zaidi ya 3700  ikivuka lengo ambapo matarajio ilikuwa ni watu 3200.

Share To:

Post A Comment: