Wednesday, 29 September 2021

Rais Samia katupa Madarasa 15,000 sisi Tukajenge vyoo na kununua Madawati

 


Nteghenhwa Hosseah, OR-TAMISEMI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewataka Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa - Alat kwenda kujenga vyoo na kununua madawati kwenye Madarasa yatakayojengwa kwa fedha za Rais Samka Suluhu Hassan.


Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akifunga Mkutano wa ALAT mapema jana tarehe 28.09.2021 kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.


Amesema Mhe. Samia Suluhu Hassan ametupa nafuu kwa kutoa fedha za  ujenzi wa vyumba vya madarasa 15,000 sasa sisi inabidi tusibweteke tuendelee na juhudi katika ujenzi wa matundu ya vyoo na ununuzi wa madawati kwa vyumba hivyo vitakavyojengwa.


Sitawaelewa madarasa haya yakikamilika

Yakose madawati na wanafunzi wasiwe na matundu ya vyoo vya kutosha msiende uko Mkarelax kazi inaendelea mkaanze kuweka mipango ya kujenga matundu ya vyoo na kunua madati.


Aidha aliwakumbusha wajumbe hao wa ALAT kuwa taarifa za mahitaji ya Halmashauri zao kiganjani ili wakati wowote zinapohitajika zitumwe haraka na sio kuchukua muda mrefu kana kwamba hawafahamu maeneo yenye uhitaji katika eneo la Afya, Elimu na Miundombinu.

No comments:

Post a Comment