Monday, 13 September 2021

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA ATANGAZWA KUWA KINARA WA KUTETEA HAKI ZA WATOTO NJITI

 

Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndugai (MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Ajenga wa Mtoto Njiti iliyofanyika Jijini Dodoma  
Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndugai (MB) akizungumza mara baada ya kufanya uzinduzi huo
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara  Neema Lugangira akizungumza wakati wa uzinduzi huo

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara  Neema Lugangira ametangazwa kuwa mmoja wa Wabunge Vinara wa Kutetea Haki za Watoto Njiti (National Champions for Rights of Premature Babies).

Hayo yalibainishwa wakati wa Uzinduzi wa Ajenga wa Mtoto Njiti iliyofanyika Jijini Dodoma kwa kuzunduliwa na Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndugai (MB) ambapo katika Uzinduzi huo Taasisi ya Doris Mollel Foundation ilimtagaza Mbunge Lugangira na wengine.

Wabunge wengine waliotangazwa kuwa Vinara wa Haki za Watoto Njiti ni Mhe Stanslaus Nyongo, Mhe Festo Sanga, Mhe Salome Makamba na Mhe Kassim Hassan Haji ambapo kupitia Agenda ya Mtoto Njiti tayari Wabunge hao :inara wameshaainisha maeneo ya kuanza kufanyia kazi.

Maeneo ambayo wataanza kufanyia kazi ni Mama anayejifungua mtoto njiti kuongezewa likizo ya uzazi, bima ya afya itambue huduma zinazohitajika kwa watoto njiti na vifaa tiba (Incubators) vipatikane hospitali zote nchini ikiwemo namna ya kufanya ulezi wa kangaroo.

Aidha pia elimu ya uzazi wa watoto njiti ijumuishwe katika elimu inayotolewa shuleni ikiwemo lishe bora kwa wakina mama wajawazito kama kinga ya kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa wakiwa watoto njiti

No comments:

Post a Comment