Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo (wa kushoto) akiteta jambo na Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Kaskazini, Arnold Mapinduzi (wa kulia) walipofika katika Kiwanda cha Sayona, KIBOKO kinachotengeneza Plastiki, Rangi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo (aliyevaa Shati Jani la Mgomba) akitoa maelekezo wa baadhi ya Wafanyakazi wa Kiwanda cha Cocacola Tanzania kilichopo Mwenge, Dar es Salaam.

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo ametoa miezi Sita kwa Kiwanda cha Sayona Drinks Ltd kuhakikisha bidhaa zake zinatafutiwa uhifadhi mzuri na hazichanganywi na bidhaa nyingine zozote ili kuwalinda kiafya Watumiaji wa vinywaji hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ziara yake ya ukaguzi wa mazingira mkoani Dar es Salaam, akiwa kwenye Kiwanda cha Sayona Drinks kilichopo Mikocheni, Waziri Jafo amesema wanafanya maamuzi hayo ili kuwalinda Watanzania kutumia bidhaa mbalimbali za Viwandani zikiwa salama bila kusababisha athari kwao.

Waziri Jafo amesema katika Kiwanda hicho cha Sayona amekutana pia na Kiwanda cha KIBOKO ambacho kinazalisha bidhaa za Plastiki, yakiwemo Matanki sambamba na Rangi za Nyumba hali inayohatarisha afya za Watumiaji wa kinywaji hicho kutokana n kuchanganywa na bidhaa nyingine katika uhifadhi wake.

“Natoa miezi Sita kwa kinywaji cha Sayona kitafutiwe sehemu yake na kisichanganywe na bidhaa nyingine katika kuhifadhi”, amesema Jafo

Pia Waziri Jafo amefurahishwa na kuwapongeza Kampuni ya Cocacola Tanzania kusimamia vizuri mazingira yake kuanzia uzalishaji wa kinywaji hicho katika kuhakikisha mifumo ya maji taka yanakuwa sehemu yake bila kusambaa kiholela na kuleta madhara kwa jamii.

Share To:

Post A Comment: