Friday, 24 September 2021

DC MBOGWE AIPONGEZA TANESCO


Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhandisi Charles F. Kabeho,akizungumza na wafanyakazi wa TANESCO mara baada ya kutembelea Banda la TANESCO kwenye Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini katika Viwanja vya Maonesho Bombambili EPZ Mkoani Geita leo September 242021.

...................................................

Na.Alex Sonna,Geita Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhandisi Charles F. Kabeho amelipongeza Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kwa kuendelea kupeleka umeme kwa wananchi na wafanyabiashara katika Wilaya yake.

Kauli hiyo ameitoa leo September 24,2021 alipotembelea Banda la TANESCO kwenye Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini katika Viwanja vya Maonesho Bombambili EPZ Mkoani Geita.

“Niwashukuru TANESCO kwa kazi kubwa mnazozifanya, mmeweza kuwapatia wananchi umeme wa uhakika katika wilaya yangu na sehemu nyingi .

“Kwa kweli mnastahili pongezi, tulikuwa katika shida kubwa ya kupata umeme wa uhakika kwa muda mrefu, lakini hali kwa sasa imebadilika sana, umeme hausumbui kama ilivyokuwa hapo awali.” amesema Mhandisi Kabeho

Hata hivyo Dc ametoa wito kwa wananchi kutembelea Banda la TANESCO ili kuja kujifunza na kujionea kifaa cha UMETA ,ambacho wataalamu wanaonyesha hatua zote kuanzia maombi ya umeme hadi hatua ya mwisho umeme unapomfikia mteja.

Maonyesho hayo yenye Kauli mbiu ya Sekta ya Madini kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu

No comments:

Post a Comment