Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro amemkabidhi Mkandarasi M/S SIMJO TECH COMPANY LIMITED Mkataba Na.AE/092/2020-2021/TAG/W/04 wenye Jumla ya Tsh 188,770,000/= na Mkataba Na.AE/092/2020-2021/TAG/W/02 wenye jumla ya Tsh.117,857,250/= wa Ujenzi wa Barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli unaohusisha Matengenezo Maalum, Matengenezo sehemu Korofi, Uchongaji kwa Greda, Kupanua kwa kukata Udongo, Kuvunja Mawe, Kuweka Changarawe na Ujenzi wa Vivuko(Kalavati na Daraja Mfuto)


Mkuu wa Wilaya ya Lushoto aliambatana na Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Injinia Theophilda N Domisian na Injinia Renatus Mkina Mhandisi wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli na Mkurugenzi wa Kampuni ya M/S SIMJO TECH COMPANY LIMITED Jones D Kavuta na Injinia Lameck Ndobo.


Pia katika kila Kata ambayo Mradi wa Barabara unapita Diwani wa Kata husika, Mtendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji na Wenyeviti wa Vijiji vilivyopitiwa na Mradi walikuwepo na kushirikishwa ili kupata Uelewa kuhusu Mradi husika.


Mikataba hii miwili ya Ujenzi wa Barabara inahusisha Matengenezo Maalum, Matengenezo sehemu Korofi, Kuchonga, Kupanua, Kuvunja Mawe, Kuweka Changarawe na Ujenzi wa Vivuko katika Mkataba Na.AE/092/2020-2021/TAG/W/04 wenye Barabara za MBELEI -BAGA - MGWASHI -MILINGANO (Matengenezo Maalum ya 13.3km) MILINGANO - YAMBA (Matengenezo Maalum 2 km), KWEULASI - KWAMKOMOLE (Matengenezo Maalum 2km), MASHEWA - MILINGANO - MLOLA (Matengenezo Maalum 2km), MILINGANO - KWEDIWA (Matengenezo Maalum 2km), MBELEI - MGWASHI - MILINGANO (Matengenezo maeneo Korofi 2km) na Ujenzi wa Kalavati na Vivuko Barabara za MBELEI - MGWASHI - MILINGANO (Kalavati la kipenyo cha 900mm mstali mmoja na Daraja Mfuto 30m2) pamoja na barabara ya MGWASHI - MALOMBOI (Kalavati za Kipenyo cha 900mm Mistali miwili) na Mkataba Na.AE/092/2020-2021/TAG/W/02 wenye jumla ya Tsh.117,857,250/= wa Ujenzi wa Barabara za FUNTA - KWEMINYASI (Matengenezo ya Kawaida 3.7 km), VULII - MAHEZANGULU - MAGOMA (Matengenezo ya Kawaida 5km) na MKAALIE - KWASHEMSHI (Matengenezo ya Kawaida 4km), BALANGAI - TAMOTA - KERENGE (Matengenezo Maeneo Korofi 2km), VULII - MAHEZANGULU - MAGOMA (Matengenezo Maeneo Korofi 2km), BALANGAI - TAMOTA - KERENGE (Matengenezo Maalum 3km) na Ujenzi wa Vivuko na Kalavati katika Barabara za VULII - MAHEZANGULU - MAGOMA (Daraja Mfuto 40m2, Kalavati la Kipenyo cha 900mm mstali mmoja), BALANGAI - TAMOTA - KERENGE (Daraja Mfuto 80m2, Kalavati la Kipenyo 900mm Mstali Mmoja) na MKALIE - KWESHEMSHI (Daraja Mfuto 60m2)


Madiwani wa Kata zinazopitiwa na Mradi huo; Diwani wa Kata ya Baga ndugu Ramadhani M Kingazi, Diwani wa Kata ya Mgwashi ndugu Salim Athumani Abdallah, Diwani wa Kata ya Milingano ndugu Leonard Peter, Diwani wa Kata ya Kwamkomole ndugu Hozza Mandia na Diwani wa Kata ya Mahezangulu ndugu Rashid Sebarua waliishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suuhu Hassani kwa kuleta Mradi huo wa Barabara kwenye maeneo yao kwani utachochea kasi ya Ukuaji wa Uchumi na Kufungua fursa za Kimaendeleo.


Pia Madiwani hao walihaidi kutoa Ushirikiano wa dhati kwa Mkandarasi huyo ili kufanikisha Mradi huo kukamilika kwa wakati na Walimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Lushoto na Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli kwa Kuwashirikisha katika hatua za awali za Utekelezaji wa Mradi huo kwani itawapa nguvu katika Usimamizi wa Mradi kama Wawakilishi wa Wananchi kwenye maeneo yao.


Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya M/S SIMJO TECH COMPANY LIMITED ndugu Jones D Kavuta alisema wamejipanga na Kuhakikisha wanamaliza kazi ndani ya muda waliopewa wa miezi 6 na kuwaomba Wananchi waweze kuwapa Ushirikiano katika Kuhifadhi Vifaa na Ulinzi wa Vifaa na alisema Kampuni yake ina Uzoefu wa kutosha katika kazi hizi na ilishafanya kazi ya Viwango kwenye Barabara ya BUMBULI - MGWASHI hivyo kama hazitatokea Changamoto za Kimazingira wanauhakika wa kukamilisha Mradi huo kwa wakati.


Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro alisema Ofisi yake kwa kushirikiana na Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli itawapa Wakandarasi hao Ushirikiano wa kutosha ili Kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na Kuzingatia Thamani halisi ya pesa inayotumika katika Mradi huo/"Value for money"

Share To:

Post A Comment: