Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro amehudhuria Misa ya Shukurani ya Father Africanus Kanju wa Shirika la Wabenedictine Ndanda Abasia baada ya kupata Upadrisho Ndanda iliyofanyikia katika Parokia ya TEKWA - Funta


Mkuu wa Wilaya ya Lushoto aliambatana na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli ndugu Hizza Mandia ambaye ni Diwani wa Kata ya Kwamkomole Wilaya ya Bumbuli.


Mkuu wa Wilaya ya Lushoto aliwaomba Waumini Kuwaombea Wanafunzi wa Darasa la Saba wanaotarajiwa kuanza Mitihani yao hivi karibuni ili waweze Kufanya vizuri katika Mitihani yao.


Pia Mkuu wa Wilaya ya Lushoto aliwaambia Mapadri na Watawa waliohudhuri Ibada hiyo kuwa Serikali inatambua kuwa Kanisa Katoliki ni Wabia wakubwa wa Maendeleo na siyo Washindani wa Serikali katika kuwaletea Wananchi Maendeleo.


Pia Mkuu wa Wilaya aliwasii Wananchi wa Wilaya ya Bumbuli kuendelea Kuchukua Tahadhari dhidi ya UVIKO-19 na Kupata Chanjo ya UVIKO-19 katika Vituo vinavyotoa Chanjo vilivyotangazwa na Serikali na kufuata maelekezo yanayotolewa na Shirika la Afya Duniani (Who), Wataalam wa Wizara ya Afya na Viongozi Waandamizi wa Serikali dhidi ya Kujikinga na UVIKO-19 na Chanjo ya UVIKO-19


Kwa upande wake Padri Africanus Kanju wa Shirika la Wabenedictine Ndanda Abasia aliwashukuru kipekee sana Wazazi wake, Sister Christa Kimashi kutoka Shirika la Mama yetu wa Usambaa, Father Joseph Sekaja wa Jimbo la Tanga, Mapadri na Watawa kwa Kushiriki katika safari yake ya kuwa Padri.

Share To:

Post A Comment: