Sunday, 15 August 2021

Naibu Waziri aungana na watanzania kuchoma Chanjo

 


Na  Mwandishi wetu,Dar


NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameungana na Watanzania kuitikia wito wa kuchanja chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19 zoezi lililozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu.


Mahundi amepata chanjo hiyo Kituo cha Jakaya kikwete kilichopiga kambi viwanja vya Farasi Oysterbay mara baada ya mbio za marathon asubuhi ziliyoongozwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ambapo pia imewekwa kambi ya kutoa chanjo.


Aidha Waziri Mkuu amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuuweka mwili katika hali ya ya utimamu.


Mwisho.

No comments:

Post a Comment