Jane Edward, Arusha


Katibu Mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki Peter Mathuki amewataka wafanyabiashara wa Afrika mashariki kufanya Kazi kwa pamoja ili kupunguza gharama na kuweka mahusiano mazuri kwa nchi za Afrika mashariki.


Mathuki ameyasema hayo wakati wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika kikao Kazi kilichowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania.


"Mimi kama katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki ninaona kikao hiki ni cha muhimu sana kwa kuwashirikisha wafanyabiashara na wadau wa sekta binafsi, ili kuona namna ya kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara hao ndani ya jumuiya hii" Alisema Mathuki


Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji baraza la biashara jumuiya ya Afrika Mashariki (EABC)John Bosco Kalisa amesema kikao hiko ni muhimu sana kwa kuwakutanisha wafanyabiashara na sekta binafsi kujadili kwa pamoja na kutoka na mitazamo ya pamoja ili kujenga baraza la biashara kwa pamoja. 


kalisa aliipongeza ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa namna wanavyoshirikiana na baraza hilo la biashara huku ikiwa lengo ni kuona biashara inafanyika bila vikwazo vitakavyokwamisha wafanyabiashara kufanya kazi ndani ya jumuiya


Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amebainisha kuwa biashara kati ya nchi hizi za jumuiya kwa takribani miezi sita zimeongezeka ambapo wakuu wa nchi pamoja na watendaji wa jumuiya hiyo wanaendelea kupambana kutengeneza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara hao.


Ameendelea kueleza kuwa Arusha kama makao makuu ya jumuiya ina changamoto kubwa sana ya kuchangamkia fursa na kuwataka wafanyabiashara kuja na majawabu badala ya malalamiko na changamoto ili kufikia malengo.


"Sisi kama serikali ya Mkoa wa Arusha tunatengeneza dawati ambalo litaweza kuwahudumia na kusaidia changamoto na sio kuweka urasimu na ucheleweshwaji wa biashara" Alisema Mongela


.....

Share To:

Post A Comment: