Katika kuhakikisha kunakuwa na uharakishwaji wa uendeshwaji wa kesi zinazohusu mirathi, talaka na zile zinazohusu Watoto,Serikali inakamilisha ujenzi wa jengo la kisasa la mahakama katika eneo la Chang’ombe wilayani Temeke litakalokuwa maalumu kwa kuendeshea mashauri hayo.

Akikagua jengo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema kukamilika kwa jengo hilo kutakuwa ni suluhisho kwa mashauri hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakicheleweshwa kutokana na Mahakama nyingi kuwa na mashauri mengine tofauti.

‘Takwimu zinaonesha kuwa Wilaya yetu ina idadi kubwa sana ya Watu na kuna wastani wa Watoto zaidi ya 100 wanaozaliwa kila siku, hii inapelekea kuwa na migogoro na kesi nyingi za mirathi, kesi za Watoto na hata talaka’-Jokate

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Wilaya ya Temeke Ilvin Mugeta, amesema ujenzi wa Mahakama hiyo utasaidia kupunguza muda wa kumaliza shauri kutoka mwaka mmoja hadi miwili ya sasa mpaka miezi sita huku akisisitiza Wananchi kuitumia miundo mbinu ya Mahakama hiyo vizuri.

Jengo hilo litakuwa la kwanza la aina yake hapa nchini ambapo kutakuwa na Mahakama ya Mwanzo, Wilaya na Mahakama kuu ambapo zitakuwa ni maalumu kwa kusikiliza mashauri yanayohusu kesi za mirathi, talaka na Watoto na linatarajiwa kufunguliwa rasmi mwezi wa tisa mwaka huu na Rais Samia Suluhu Hassan

.

.

.

.

.

.

.

S
Share To:

Post A Comment: