Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen Akizungumza na Wananchi na mabalozi wa Kata ya Namanga katika Kitongoji cha Kisongo Mlimani.

Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen Akikagua Jengo la bweni la Wavulana katika Shule ya Sekondari ya Namanga Jengo linalogharimu Zaidi ya milioni 100 Hadi kukamilika ambapo mpaka sasa limegharimu milioni 62,huku milioni 20,zikichangiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Longido na Milioni 42 zikiwa ni nguvu kazi za Wananchi,Ambapo hadi kukamilika Jengo hilo ambalo litalaza wanafunzi zaidi ya Mia moja (100).
Kutoka Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Arusha Ndugu Robert Kaseko akiwa na Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Longido wakiteta jambo na Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Profesa Rizick Shemdoe mapema hii leo Wilayani Longido alipopita kuwasalimia katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Prof. Mdoe yupo Arusha kwa ziara ya kikazi.
Katibu wa Ccm Mkoa wa Arusha Ndugu Mussa Matoroka akiwa ameambatana na Katibu wa Ccm Wilaya ya Longido Ndugu Ezekiel Mollel wakikagua Mradi wa maji wa Malisho ya wanyama ambao unakabiliwa na tozo kubwa ya maji kwa wananchi hao.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Ndugu Zelothe Stephen Zelothe wakikagua Jengo la Maabara ya Phizikia katika Shule ya Sekondari ya Namanga ambayo yenye wanafunzi 998,huku wavulana wakiwa 483 na wasichana 515.
Wajumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Arusha ikiongozwa na Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wakikagua ujenzi wa madarasa mawili yaliyogharimu milioni 50,zilizogharimu nguvu za wananchi wa Kata ya Namanga na Kata ya Kimokowa.

Na Imma Msumba, Longido

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Ndugu Zelothe Stephen Zelothe amewataka viongozi wote wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Longido kuendelea kudumisha umoja,mshikamano na Upendo lengo likiwa ni kuendeleza ufanisi wa kazi na kutetea Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Akizungumza katika ziara yake ya Mkoa iliyoanza leo katika Wilaya Longido itakayojumuisha Wilaya zote saba za Chama Mkoa wa Arusha Mwenyekiti wa Ccm Mkoa amewataka watendaji wote wa Kata na Serikali za Mitaa,Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi Mtendaji,na Mwenyekiti wa Halmashauri kuendelea kushirikiana ili kuweza kuleta tija ya maendeleo kwa wananchi na kufanikisha vyema kutangaza Chama cha Mapinduzi.

Katika ziara hiyo ya kuimarisha shughuli za Uhai wa Chama katika ngazi ya mashina Mwenyekiti wa Ccm Mkoa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya siasa Mkoa Ndugu Robert Kaseko,Neema Mollel na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (MNEC) Dkt. Daniel Pallangyo ambapo katika shughuli ya kuimarisha Uhai wa Chama na Jumuiya wamekutana na Viongozi wa Mashina,na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM huku wakikutana na makundi mbalimbali ya Wazee,Wanawake na Vijana.

"Wanachama wenzangu niwasisitize kubadilika kwani kwenye Chama chetu kumekuwa na tabia ya safu,kupangana safu ili wa chini wamchague wa juu,huu sio utaratibu wa chama chetu cha Mapinduzi,utaratibu ni kufuata Katiba,Kanuni na miongozo ya chama katika kuwapata viongozi sahihi wa chama" Zelothe Stephen

"Mimi kama Mwenyekiti nipende kumpongeza Mbunge wenu Kiruswa kazi yake ya kutembelea wananchi na yaliyopitishwa kwenye bajeti ambayo yanayowagusa,niwaombe mkae na madiwani mpange ratiba ya ziara zenu za kuwasikiliza wananchi hawa" Zelothe Stephen

Kwa upande wake Katibu wa Ccm Mkoa wa Arusha Mussa Matoroka amewataka wanachama wa Ccm kuwa wabunifu katika kufanikisha masuala mbalimbali ya wananchi kwa ubora ,ili kufanikisha uchaguzi Mkuu wa Chama mwakani 2022

Share To:

Post A Comment: