Friday, 9 July 2021

Wananchi Washangaa Waziri Ummy kufika Kalya awa Waziri wa kwanza tangu uhuru

  


Na. Angela Msimbira  Kalya – KIGOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu afika Kata ya Kalya km 300 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Uvinza, wananchi Washangazwa kumwona wasema hawajawahi kumwona waziri toka Uhuru.

Waziri Ummy amefanya ziara hiyo kwa lengo la   kukagua miradi ya elimu na afya  na  kuwahamasisha watumishi  wa TAMISEMI hasa waalimu na watumishi wa afya  wanaofanya  kazi katika kata  ambazo ni ngumu  kufikika na kutoa hamasa kwa watumishi hao kufanyakazi kwa weledi katika kutoa huduma bora kwa jamii.  

Wananchi wamemshukuru Waziri Ummy kwa kusikia kilio chao ambapo serikali kupeleka kupeleka shilingi milioni 90 za kukamilisha  maabara 3, shule ya Sekondari Kalya, katika mwaka wa fedha 2021/2022. 

Ameendelea kufafanua kuwa kwa upande wa elimu serikali itakamilisha maboma saba ya vyumba vya madarasa kwa shule za Msingi katika kata hiyo ambapo kila boma litagharimu kiasi cha shilingi milioni 12 

Waziri Ummy amesema katika kituo cha afya cha Kalya Serikali itaongeza wodi 3 ambazo ni wodi ya wanawake, wodi ya wanaume na wodi ya watoto na kujenga chumba cha mionzi na kununua mashine ya Xray ambapo kwa sasa wananchi wanafuata huduma ya mionzi katika Hospitali ya Mkoa wa Kigoma ambapo ni umbali wa kilometa 300 kutoka kata ya karya.

Aidha, Waziri Ummy ameahidi kupeleka  bilioni 1.5 kwa ajili ya kuboresha  barabara zinazosimamiwa na Tarura  kutoka Kalya kupitia Ubanda- Katente hadi  katavi ili kuwawezesha wananchi  kusafirisha  kwa urahisi mazao  yao hususani mpunga na mahindi. 

Wakati huohuo Diwani wa Kata ya Kalya Mhe. Jackson Mateso amemshukuru Waziri Ummy kwa kuwa waziri wa kwanza kutembelea katika kata ya Kalya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza tangu uhuru ambapo hata mwenge wa uhuru haujawahi kumfikia.

No comments:

Post a Comment