Friday, 9 July 2021

Vikundi 12 vyanufaika na mkopo wa shilingi milioni 110

  


Halmashauri ya Wilaya Uvinza


Na Angela Msimbira UVINZA - KIGOMA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu aipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza kwa kutekeleza agizo la Serikali ya kutenga  asilimia kumi ya Fedha za Maendeleo kwa ajili ya Mikopo ya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu


Akikabidhi mfano wa hundi kwa  Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu Waziri Ummy ameziagiza Halmashauri zote nchini  kuacha kutoa mikopo midogo midogo  kwa kuwa vikundi vingine vina uwezo wa kufanya biashara kubwa na kufanya marejesho kwa wakati na waweze kujikwamua kiuchumi.


Waziri Ummy amesema amevitaka vikundi  vyote vya ujasiriamali vinavyopatiwa mikopo kurejesha kwa kuwa mikopo hiyo si hisani bali ni fedha ambazo zinahitajika wananchi wengine kupatiwa mikopo.


 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza  katika Mwaka wa Fedha wa 2013/2014 hadi  2020/2021  vikundi  64 vya wanawake  vimenufaika na mikopo zaidi ya  milioni 313, vikundi 39 vya vijana  vimenufaika na mikopo ya zaidi ya shilingi 219 na  vikundi 8 vya  watu wenye ulemavu  vimenufaika na mikopo yenye  zaidi ya shilingi milioni 51 hivyo kufanya jumla ya mikopo iliyotolewa ni  zaidi ya shilingi milioni 583. 


Aidha, Jumla ya Mikopo yote iliyotolewa  na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza  kwa mwaka wa Fedha 2020/2021  ni shilingi milioni 194 ambazo zinajumuisha asilimia 10 ya mapato ya ndani  ambayo ni shilingi milioni 124 na fedha za marejesho  milioni 70

No comments:

Post a Comment