Wednesday, 14 July 2021

TRUMP awakumbuka Wajawazito Hospitali ya Mkoa Manyara.

 


Na John Walter-Babati

Wafanyabiashara na wadau mbalimbali wilayani Babati mkoa wa Manyara wameombwa kusaidia wagonjwa na watu wenye mahitaji maalum vifaa maalumu vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya COVID 19  ili kuunga mkono juhudi za serikali katika udhibiti.

Hayo yamesemwa na Gabriel  Nyange Maarufu Trump mdau wa maendeleo kutoka Magugu alipotembelea wagonjwa Katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara ambaye ameamua kushiriki kuwapa pole kwa kuwapa vitakasa mikono,sabuni,pampasi za watoto na vinywaji  baada ya kuguswa na utendaji wa utawala wa  awamu ya sita.

Trump amesema lengo la kutoa msaada huo kwa wakina mama wajawazito na watoto ni kuwafariji na kuwapa tabasamu.

Hata hivyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Wa Manyara Dr.Catherin Magali amesema suala la kutoa msaada kwa wagonjwa linaleta tabasamu,matumaini mapya kwao,hivyo wadau wengine watumie nafasi walizonazo kusaidia wajawazito,watoto na wagonjwa wengine kama alivyofanya Nyange (TRUMP).

No comments:

Post a Comment